Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu wa Canada kwa ushirikiano na The Canadian Comprehensive Auditing Foundation - La Fondation Canadienne Pour la Verification Integree (CCAF - FCVI Inc.), kwa pamoja wameandaa hafla ya kutangaza vivutio vya utalii vya nchi za Tanzania, Senegal na Ghana. 
 Hafla hiyo iliyofanyika katika Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu wa Canada pia imedhaminiwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Canada. 
 Katika hafla hiyo ambayo iliambatana na utoaji wa mada juu ya utamaduni na utalii, Tanzania iliwakilishwa na Bi. Ndyanao Mgweno na Bwana Andrew Kellei ambao wanatoka katika Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wa Tanzania. 
Maafisa hao wako nchini Canada kwa mafunzo ya Ukaguzi wa ufanisi (performance Audit) ambayo yanatolewa na Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu wa Canada. Shughuli za kutangaza utamaduni wa Utalii wa Tanzania ilisimamiwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Canada ambapo Mheshimiwa Balozi wetu huko Canada Mhe. Jack Zoka aliwakilishwa na Kaimu wa Kitengo cha Utalii na Mwambata wa Fedha wa Ubalozi huo Ndg. Richard Masalu. 
 Banda la Tanzania limetia fora kwa vielelezo na vivutio vya utalii kati ya mabanda mengine kama inavyoonekana katika picha.
Kutoka kulia  ni Bi. Ndyanao Mgweno kutoka Ofisi ya Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali Tanzania akiwa amebeba mtoto wake ambaye ni mualikwa katika shughuli hiyo, katika ni Ndg. Richard Masalu aliyemwakiliswa Balozi wetu nchini Canada, akifuatiwa na Ndg. Andrew Kelei ambaye pia anatoka Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Tanzania. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Yohannes E.K.April 14, 2015

    Hongereni sana ndugu. Ni masuala ya ubunifu kidogo tu. Vitu ni vingi Tanzania. Inapendeza sana!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...