
Rushwa ya ngono
pamoja na matumizi mabaya ya madaraka yametajwa kuwa ni moja kati ya matatizo
makubwa ambayo yamezidi kuweka mizizi nchini tanzania na kuwaadhiri wasichana
wengi huku sheria ikishindwa kuweka wazi adhabu mahususi ili kuwabana
wanaohusika katika swala hilo.
|
Hayo
yamesemwa leo jijini dare s salaam na Jaji mstaafu wa mahakama ya rufaa nchini
tanzania mama EUSEBIA MUNUO wakati akiendesha mafunzo maalumu kwa wanafunzi wa
chuo kikuu cha Dar es salaam mafunzo yaliyolenga kuzungumzia madhara na jinsi
rushwa ya ngono inavyoathiri kizazi kukubwa cha wasichana wa sasa nchini
tanzania.
Amesema kuwa tatizo la
ruswa ya ngono limekuwa likiongezeka siku hadi siku nchini kutokana na kutokuwa
na sheria mahususi ambayo inawaadhiu moja kwa moja wahusika katika swala
hilo.
Amesema kuwa wasichana
wengi wanapokuwa katika harakati za kutafuta ajira katika maofisi mbalimbali
wamejikuta wakitumia miili yao kuwashawishi mabosi wao ili waweze kupata ajira
jambo ambalo amesema kuwa sio sahihi na wasichana hao wamekuwa wakikosa msaada
kuhusu swala hilo.
Amesema kuwa
hata katika maofisi mbalimbali kumekuwa na wasichana ambao hawana vigezi vya
kuwa katika maofisi hayo ila wapo tu kwa sababu wanatembea na mabisi wao jambo
ambalo limetajwa kuleta madhara makubwa ikiwemo kushusha ufanisi wa kazi pamoja
na ofisi husika kwa ujumla.
|
Mwanafunzi
CATHERIN OLOMY akizungumza na mwandishi wa mtandao huu juu ya mafanikio
ya semina hiyo ya siku moja kwao na kwa jamii kwa ujumla
|
Baadhi
ya wanafunzi ambao wamehuduria mafunzo hayo ya siku moja ambayo
yameandaliwa na WILAK kwa kushirikiana na TAWLA mwanafuzni CATHERINE
OLIMY ambaye ni mmoja ya washiriki anasema kuwa mafunzo hayo ni muhimu
sana kwa wanafunzi wa sasa hususani wasichana kwa kuwa yatawasaidia
kujiamini kujua haki zao kama wanafunzi na watoto wa kike,ikiwa ni
pamoja na kujua udhamani wao pindi wanapokutana na swala la rushwa ya
ngono.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...