Na Avila Kakingo Globu ya jamii
MAMLAKA ya mawasiliano Tanzania (TCRA) wamekanilisha mfumo wa kidijitali kwa nchi nzima.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Meneja Mawasiliano wa mamlaka hiyo, Innocent Mungy, amesema Tanzania imekuwa nchi ya kwanza kutekeleza maazimio ya nchi zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara (SADC ) na yale ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Amesema mfumo wa analojia ulizimwa rasmi Desemba 31,2012,kwa mujibu wa makubaliano ya nchi mwanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo tulianza kuzima mitambo hiyo na kuwasha ya dijitali kwa baadhi ya mikoa hapa nchini.
Mungy amesema mpaka sasa mikoa yote ya Tanzania inatumia mfumo wa kidijitali ambapo inatumia mifumo minne tofauti ambayo ni Satelaiti, mfumo wa mitambo ya utangazaji kupitia kebo,mfumo wa utangazaji wa dijitali kwa mitambo iliyosimikwa juu ya ardhi pamoja na mfumo wa utangazaji wa intaneti.
Meneja Mawasiliano wa mamlaka ya mawasiliano (TCRA), Innocent Mungy (katikati) akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo juu ya mafanikio waliyoyapata katikmfumo wa Dijitali.Kushoto ni Mhandisi wa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) Christopha Assenga na kulia Semu Mwakyanjala Afisa Mawasiliano mkuu TCRA.
Hongera TCRA
ReplyDelete