Marehemu Dkt. Alec
Chemponda enzi za uhai wake
Mwenyekiti Mtendaji wa Michuzi Media Group anaungana na familia, ndugu, jamaa, jirani na marafiki wa Chemponda katika kuomboleza kifo cha Dkt Alec Che Mponda kilichotokea juzi Machi 30, 2015 katika hospitali ya Massana jijini Dar es salaam kutokana na saratani (cancer) ya mifupa iliyokuwa ikimsumbua kwa muda mrefu. Alikuwa na umri wa miaka 80.
Tunatoa mkono wa pole kwa binti mkubwa wa marehemu na blogger na mwanahabari mwenzetu, Bi Chemi Che-Mponda pamoja na wadogo wake wote na wajukuu wa marehemu ambaye atakumbukwa kuwa mmoja wa wanasiasa wakongwe nchini aliyepata kuanzisha na kuongoza chama cha Tanzania People'e Party (TPP).
Mbali na siasa pamoja na kuwa mmoja wa watangazaji wa kwanza wa Idha ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika (VOA) Marehemu Dkt Che-Mponda pia aliandika thesis ya shahada ya uzamivu (PhD) juu ya mzozo wa mpaka wa Tanzania na Malawi ambayo imesimama kama kimoja ya kielelezo muhimu katika swala hilo nyeti.
Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu Mbezi (mbele ya Massana Hospital) jijini Dar es salaam.
Mola aiweke roho ya marehemu
mahala pema peponi
Amen
Pole Chemi na Jessica. mungu amlaze mzee mahali pema peponi. Amina.
ReplyDeletePoleni wafiwa Mungu awatie nguvu wakati huu mnapoomboleza kuondokewa na mpendwa wenu.
ReplyDelete