JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA
YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu zoezi linaloendelea kuhusiana na Vyama
vya Kijamii vilivyosajiliwa chini ya Sheria ya Vyama, Sura 337 kuwa ni la kubaini
vyama vile ambavyo havitekelezi matakwa ya kisheria ya kuwasilisha taarifa za
mwaka za ukaguzi wa hesabu za vyama husika na pia vile ambavyo havilipi ada ya
mwaka kama sheria ya Vyama inavyoelezea.
Vyama
ambavyo vitabainika kukiuka matakwa ya kisheria kama yaliyotajwa hapo juu ndio
vitakavyofutwa kutoka katika Daftari la Msajili wa Vyama vya Kijamii. Orodha ya Vyama vitakavyofutwa itaanza
kutolewa kwa awamu kuanzia wiki hii na kwa kuanzia, orodha hiyo itahusu Vyama
vilivyosajiliwa mkoni Dar es Salaam.
Kufuatana
na orodha tuliyonayo kiasi cha vyama 10,000 vya Kijamii na Taasisi za Dini vimesajiliwa
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na vitakavyofutwa ni vile tu ambavyo haviwasilishi
taarifa za kila mwaka za ukaguzi wa hesabu zao na pia kama havilipi ada ya kila
mwaka kama sheria inavyotaka. Hii ina
maana kuwa vile ambavyo vinatekeleza matakwa hayo ya kisheria havitafutwa.
Kwa
taarifa hii napenda kueleza kuwa sio Vyama vyote vya Kijamii na Taasisi za Dini
vitakavyofutwa na wala hakuna mpango wa kuanza upya zoezi la Usajili wa Vyama
vya Kijamii.
Aidha
ni vyema ikaeleweka kuwa zoezi linaloendelea kwa sasa halihusiani na Taasisi
zinazoelezewa kujiingiza katika masuala ya kisiasa na pia ieleweke kuwa Wizara
yetu haihusiki na usajili wa NGO.
Imetolewa na Isaac J. Nantanga
MSEMAJI WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...