Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, kwa mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 4(1) cha Sheria ya Korosho ya mwaka 2009 (Sura ya 203 ya Sheria za Tanzania), amemteua Mhe. Anna Margareth Abdallah (MB) kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Korosho.
Aidha, Mhe. Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika amewateua wafuatao kuwa wajumbe wa Bodi hiyo ya Wakurugenzi kwa mujibu wa kifungu cha 4(1) cha Sheria ya Korosho ya mwaka 2009 (Sura ya 203 ya Sheria za Tanzania):-
1. Joseph Florian Haule - Mwakilishi wa wabanguaji korosho nchini.
2. Bw. Thomas Chatanda - Mwakilishi wa wakulima wa korosho
3. Mhe. Mudhihir M. Mudhihir- mtaalamu mwenye uzoefu kwenye sekta ya korosho
4. Bw. Rashid M. Serungwi- Mwakilishi wa wakulima wa korosho
5. Dkt Louis Kagusa - Mtafiti wa Korosho, anayewakilishwa watafiti wa korosho
6. Bw. Mwinyikondo Lila - Mtaalamu mwenye uzoefu kwenye sekta ya korosho
7. Bw. Edgar Maokola Majogo - Mwakilishi wa wabanguaji wa korosho
8. Bibi Belinda P. Kyesi - Mwakilishi wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika.
Uteuzi huu ni wa miaka mitatu na unaanza rasmi tarehe 23 Februari, 2015.
IMETOLEWA NA:
Sophia E. Kaduma
KATIBU MKUU
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...