Naibu waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mhe. Dkt. Pindi H. Chana (MB) azindua rasmi Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto mkoani Morogoro tarehe 9 Aprili, 2015. Baraza hili linafanya kikao chake cha siku mbili kuanzia tarehe 9 hadi 10 Aprili, 2015.

Baraza la Wafanyakazi linaundwa na wawakilishi wa wafanyakazi wote wa Wizara na wanachaguliwa kwa mfumo wa haki na uwazi. Baraza hili ni chombo muhimu sana kwani uhalali na uundwaji wake upo kisheria. Madhumuni yake ni kuishauri Serikali katika ngazi ya Wizara na taasisi kuhusu usimamizi wa kazi, mwenendo wa utendaji wa kazi na Rasilimali watu ili kuleta tija katika sehemu ya kazi. Kubwa zaidi ni kuongeza kasi ya kuwahudumia wananchi.

Ni kupitia Baraza hili ambapo mwajiri hupata maoni ya watumishi na kuungana nao katika kujadili na kupitisha kwa pamoja maazimio ya utekelezaji kuhusu masuala yanayoihusu Wizara ili kuleta tija.

Mhe. Dkt. Pindi H. Chana amesisitiza kuwa Sekta ya Maendeleo ya Jamii ni muhimu katika uchumi wa nchi na ustawi wa jamii zetu kwa kuwa shughuli zake zinagusa moja kwa moja maisha ya kila siku ya jamii iwe katika maeneo ya mijini au vijijini.

Kutokana na ukweli huu na umuhimu wa sekta Baraza hili linatakiwa kujua kwa undani mafanikio, fursa na changamoto zinazoikabili Wizara na kushauri njia za kuleta ufanisi na kutatua matatizo yanayojitokeza kwa kutumia sera na sheria za Wizara na za nchi kwa ujumla.
Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto wakiwa katika Uzinduzi wa baraza hilo mkoani Morogoro tarehe 9 Aprili, 2015.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto katika picha ya pamoja na Naibu waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mhe. Dkt. Pindi Chana (MB) (waliokaa katikati), Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Dkt Rajabu Rutengwe (wa pili kulia), Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro Bw.Noeli Kazimoto (wa kwanza kulia), katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Bibi Anna Maembe na naibu wake Bibi Nuru Millao (kushoto kwa Naibu waziri) mkoani Morogoro tarehe 9 Aprili, 2015. Picha na Hassan Mabuye

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...