VIONGOZI wa Klabu ya Coastal Union wamewatakiwa kushikamana vilivyo ili kuweza kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri katika michezo yao iliyosalia katika Michuano ya Ligi kuu soka Tanzania Bara. 
 Wito huo ulitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Magalula Saidi wakati alipokutana na viongozi wa timu hiyo ofisini kwa lengo la kufahamiana ambapo Makamu Mwenyekiti wa Coastal Union, Steven Mguto aliwaongozwa viongozi wengine kwenye kikao hicho.
 Alisema kuwa muda uliobakia kwenye mechi za Ligi kuu sio wa kuanza kufikiria ni kitu gani kimetokea bali ni kuweka mipango imara na madhubuti itakayowapa mafanikio ili waweze kujipanga msimu ujao kwa ligi nyengine. Aidha aliwataka viongozi hao kujiepusha na migogoro, mifarakano iliyokuwa na tija kwani hali hiyo ikiruhusiwa itashindwa kuwapa maendeleo na kukwamisha mipango yao waliojiwekea. 
 Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Coastal Union, Steven Mguto alimuhaidi mkuu wa mkoa huyo kuyafanyia kazi kwa asilimia kubwa maelekezo aliyoyatoa ili waweze kupata mafanikio.. 
 Naye, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Coastal Union, Akida Machai alisema changamoto zilizojitokeza kwenye michuano hiyo watazifanyia kazi kwa umakini mkubwa ili ziweze kuleta ufanisi katika michezo iliyosalia. 
 Kikao hicho kilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa soka akiwemo Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya shirikisho la soka Nchini (TFF) Khalid Abdallah.
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Magalula Saidi (katikati waliokaa)  akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Coastal Union na viongozi wa mkoa,kushoto kwake ni Makamu Mwenyekiti wa Coastal Union,Steven Mguto
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Coastal Union,Akida Machai akimuelezea mikakati ya timu hiyo mkuu wa Mkoa wa Tanga Magalula Saidi wakati wa kikao cha pamoja baina ya viongozi wa Coastal Union na Mkuu huyo wa mkoa kwa lengo la kufahamiana.  Imetolewa na Kitengo cha Idara ya Habari na Mawasiliano,  Coastal Union.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Goli Nane si Mchezo....Hadi Mkuu wa Mkoa kawaita!!! YANGA WAUAJI!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...