Baada
ya huduma za Kilimo Klub,M-Pesa na M-Pawa zinazotolewa na kampuni ya
mawasiliano ya Vodacom Tanzania
kuonyesha mafanikio makubwa ya kutumia mapinduzi ya teknolojia ya simu
za mkononi kuleta mabadiliko kwenye jamii,hivi sasa kampuni imejipanga
kupeleka na kuboresha huduma za mawasiliano vijijini ili ziweze
kuwafikia watanzania wengi.
Hayo
yamebainishwa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano Kampuni
hiyo,Rosalynn Mworia kufuatia kampuni
hiyo pamoja na makampuni mengine yanayotoa huduma za simu nchini
TTCL,Tigo na Airtel kusaini mkataba na Mfuko wa Kuendeleza Mawasiliano
Vijijini (UCAF) hivi karibuni ambapo itatakiwa kupeleka huduma katika
kata 36 vijijini na vilevile imesaini mkataba wa kupeleka
huduma za mawasiliano sehemu za mipakani mwa nchi.
“Mawasiliano ni jambo la msingi katika kuleta mabadiliko na kuendeleza jamii kama ambavyo tumeshuhudi.
maisha ya watanzania yamerahisishwa tangu kuboreshwa huduma za
mawasiliano hususani kuingia kwa makampuni yanayotoa huduma za mkononi
ambayo yamekuwa na ubunifu mkubwa wa huduma za kurahisisha maisha ya
kila siku ya wananchi”.Alisema.
Aliongeza kuwa huduma hizi ni muhimu kuwafikia watanzania wote hususani waishio maeneo ya vijijini na ndio
maana Vodacom siku zote ambayo mtandao wake unawafikia watanzania wengi na zaidi ya asilimia 45
ya minara yake ikiwa imejengwa maeneo ya vijijini itaendelea kuunga
mkono jitihada za serikali za kuboresha mawasiliano ya simu katika
huduma za vijijini na kubuni huduma zitakazoweza
kuleta mabadiliko vijijini.
Alizitaja baadhi ya huduma za Kilimo Klub,M-Pawa na M-Pesa zinazotolewa na kampuni hiyo kuwa zinaendelea kuleta
mabadiliko makubwa kwenye jamii ya watanzania na kuboresha maisha yao kuwa murua. “Tuna
imani huduma hizi na nyingine tutakazoendelea kuzibuni zitaleta
mabadiliko kwa watanzania wengi hususani wenye kipato cha chini hususani
wakulima na kuwatoa katika hali
ya chini na maisha yao kuwa bora zaidi”.Alisisiza.
Hivi Karibuni Naibu Waziri wa Kilimo,Chakula na Ushirika Mh.Godfrey Zambi alisema kuwa huduma zinazolenga kuboresha
maisha ya wakulima vijijini kama ilivyo huduma ya Kilimo Klub
ni muhimu sana kwa jamii ya watanzania ambao asilimia kubwa ni wakulima
na wanaishi maisha ya vijijini wakiwa na maisha duni kiasi cha
kutojitosheleza kwa mahitaji yao muhimu.
Huduma ya kilimo inawawezesha wakulima kupata taarifa mbalimbali kuhusu shughuli zao za ukulima kupitia simu
zao za mkononi ambapo vilevile wanaweza kutuma na kupokea
fedha,
kufanya mihamala ya malipo kupitia huduma ya M-Pesa na wanaweza
kujiwekea akiba na kupata mikopo rahisi na yenye masharti nafuu kupitia
huduma ya M-Pawa ya Vodacom
kwa kushirikiana na Benki ya CBA ambayo inaendelea kupata umaaruufu
mkubwa siku hadi siku
Huduma hii
inayolenga kubadilisha maisha ya mamilioni ya watanzania inatolewa na Vodacom pekee
kwa kushirikiana na taasisi za , Olam International, Connected Farmers Alliance na Techno Serve .

Ofisa
Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Georgia
Mutagahywa (wa pili kutoka kulia) akisaini mkataba wa miradi miwili ya
upelekaji mawasiliano vijijini
awamu ya 2A kati ya Mfuko Wa Mawasiliano Kwa Wote (UCSAF)na kampuni za
simu za mkononi katika hafla iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Miradi hiyo ni upelekaji wa mawasiliano mipakani na maeneo maalum na
mradi wa kuunganisha Intaneti kwenye Shule za Umma,wengine
ni mwakilishi wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania (wa
kwanza kulia), Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya simu za mkononi ya MIC
Tanzania (Tigo) Cecilia Tiano (wa pili kutoka kulia) na Mkurugenzi Mkuu
wa Mfuko Wa Mawasiliano Kwa Wote (UCSAF) Eng. Peter
Ulanga (wa tatu kulia)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...