Mtaalamu wa Afya ya Uzazi kutoka  chama cha Uzazi na Malezi Bora Tanzania Mkoa wa Mwanza  Bi,Jacinta Mutakyawa (Aliyesimama)  akiongea na waratibu wa Ukimwi,Maafisa Vijana na Wadau mbalimbali juu ya haki za Afya ya Uzazi na Ujinsia leo jijini Mwanza.Haki izo zikiwemo haki ya kuwa huru  dhidi ya vitendo vya ukatili na haki ya kuchagua na kupanga uzazi.


Mratibu wa Ukimwi kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Bw,Musa Varisanga(Aliyevaa Miwani)  akifurahia jambo na Mratibu wa Vijana kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania Bi,Grace Kessy(wa Kwanza Kulia)  leo jijini Mwanza inapofanyika Warsha ya Stadi za Maisha na Afya ya Uzazi  katika hoteli ya Midland.
 Washiriki  wa warsha ya stadi za maisha na afya ya uzazi  wakimsikiliza kwa makini mtaalamu wa afya ya uzazi(hayuko pichani)  kutoka Mwanza Bi,Jacinta Mutakyawa alipokuwa akiwapa elimu ya Afya ya Uzazi ikijumuisha Afya ya Ujinsia na Haki zake leo jijini Mwanza  katika hoteli ya Midland.Warsha iyo imefikia siku ya Pili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...