
Akizungumza katika mkutano wa wanachama uliofanyika mwishoni
mwa wiki Dar es Salaam, Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib alisema
maandalizi ya wasanii hao kuhamia kijijini yamekamilika na akiwemo yeye
ataongoza msafara huo.
Alisema kati ya wasanii watakaohamia kijijini ni mchezaji wa
zamani wa Simba, Dua Said na mwigizaji wa Bongo Movie, Lumola Matovola
‘Big’ na wengine. Taalib alisema wasanii wengine katika kikosi chao wapo wapiga
picha, walimu wa kutunga hadithi na wasanii watakaocheza filamu na
tamthilia hizo. Alisema wasanii hao pia watagaiwa mashamba ya kulima bustani za
mboga mboga, matikiti maji, pilipili na kufuga kuku, bata na mbuzi.
Katika mkutano huo ulihudhuriwa na wanachama zaidi ya 200 ilitolewa ofa ya kuingia wanachama katika kusherekea miaka 10 ya SHIWATA ambayo kilele chake kinafanyika Juni mwaka huu ambako nyumba 30 zitagaiwa.Kijiji cha Wasanii Mkuranga mpaka sasa kimejengwa nyumba 134.
Wanachama hao pia waliwataka wenzao zaidi ya 8,000 kupiga
ndiyo za kwenye kura ya maoni ya katiba mpya kwa vile imelenga
kuwakomboa wasanii kutoka kwenye wimbi la umasikini.
Mkutano huo pia ulipitisha adhabu ya kuwafukuza wanachama
ambao watakwenda kinyume na utaratibu wa uliowekwa wakati wa kujiunga
uanachama, usimamizi wa mashamba na kukiukwa kwa sheria za kijiji cha
wasanii Mwanzega, Mkuranga.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...