Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji) Mhe. Mhandisi
Christopher Chiza (Mb) ahudhuria Kongamano Kubwa la Biashara kati ya Comoro na
Tanzania, litakalofanyika tarehe 23 Aprili, 2015 Visiwani Comoro.
Lengo kuu la kongamano hilo ni “kuongeza kiwango cha biashara na uwekezaji kati ya
Tanzania na Comoro kwa kutambua fursa zilizopo kati ya nchi hizi mbili na kurasimisha
biashara ambayo kwa sasa hairatibiwi”.
Kongamano hilo ambalo litawakutanisha viongozi, maafisa wandamizi wenye dhamana
ya kuendeleza biashara kutoka Tanzania na Comoro pamoja na wadau wa Sekta
Binafsi, litafungua rasmi fursa ya kutangaza na kuuza bidhaa zinazozalishwa Tanzania
kwa wafanyabiashara watakaopenda kufanya hivyo kutokana na nafasi nyingi za
biashara na uwekezaji zilizopo katika Visiwa vya Comoro.
Miongoni mwa mada ambazo zitazungumzwa katika kongamano hilo ni pamoja na;
Mada kadhaa kuhusu fursa za biashara na uwekezaji nchini Tanzania na Comoro,
mazingira ya biashara za uwekezaji nchini Tanzania na Comoro, fursa zinazopatikana
katika nchi hizo na usaidizi wa kiserikali katika kurahisisha baishara. Aidha, itakuwapo
fursa ya mazungumzo ya kina kati ya wafanyabiasha wa Comoro na Tanzania (business
to business discussions).
Aidha, zipo fursa nyingi za uwekezaji katika uzalishaji na usindikaji wa bidhaa za kilimo,
pamoja uwekezaji katika sekta ya huduma za afya, elimu, mawasiliano na nishati
endapo fursa hizi zitatangazwa na kuwekwa miundombinu ya uhakika ya usafiri kati ya
Tanzania na Comoro bidhaa za Tanzania zitapata soko la uhakika visiwani Comoro.
Kongamano hilo linatarajiwa kuhudhuriwa na wafanyabiashara na wadau mbalimbali
kutoka Tanzania, limeandaliwa na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania nchini
Comoro, kwa kushirikiana na kampuni ya 361 degrees ya Dar es Salaam.
Kwa
kuwashirikisha wadau mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Mamlaka ya Uendelezaji wa
Biashara Tanzania (TANTRADE) ambao wanahamasisha na kuwakaribisha
wafanyabiashara wa Tanzania, Exim Bank, Shirika la Ndege la Air Tanzania, Jumuiya ya
Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Wakulima ya Comoro (UCCIA); na Mamlaka ya
Kuendeleza Vitega uchumi vya Comoro (INM).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu( Uwekezaji na Uwezeshaji) Mhe. Mhandisi Christopher Chiza (Mb)
akibadilishana mawasiliano na baadhi ya wafanyabiashara waliowasili Visiwa vya Comoro kwa ajili ya
kushiriki katika Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Comoro, linalotarajiwa
kufanyika tarehe 23 Aprili, 2015. Kushoto (mwenye miwani) ni Balozi wa Tanzania Visiwa vya Comoro Bw.
Chabaka Kilumanga.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu( Uwekezaji na Uwezeshaji) Mhe. Mhandisi Christopher Chiza (mwenye tai) akishiriki kucheza ngoma ya asili ya Comoro mara baada ya kuwasili visiwani humo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...