Waziri wa Maiasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na Katibu Mkuu wa wizara
hiyo Dk Adrehem Meru, wakipata maelekezo kuhusiana na mipaka ya hifadhi
ya Taifa ya Saadan kutoka kwa Mhifadhi Mkuu wa Saadan, Alhaj Hassan
Nguruma (katikati) walipotembelea kutatua mgogoro uliohusu wananchi na
hifadhi hiyo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na Katibu mkuu wake
Adrehem Meru wakiwa katika boti katika mto wami juzi walipotembelea
hifadhi hiyo kwa ajili ya kutatua mgogoro wa mpaka katika ya hifadhi
hiyo na wananchi.
Mhifadhi Mkuu wa Saadan, Alhaj Hassan Nguruma(katikati) akitoa maelezo
kwa Waziri wa Maiasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na Katibu Mkuu wa
wizara hiyo Dk Aderehem Meru kuhusiana na mogoro wa mipaka baina ya
hifadhi hiyo na wawekezaji wa shamba linalopakana na hifadhi hiyo.
Waziri Nyalandu aliamuru mipaka ya zamani izingatiwe ili kumaliza
mgogoro huo.
Waziri wa Maliasili na utalii Lazaro Nyallandu na Katibu mkuu wake
Adrehem Meru wakikagua mto Wami ambao awali ulikuwa mpaka wa Hiadhi ya
Saadana na kupanuliwa kitu kilichosababisha kuwapo kwa mgogoro wa muda
mrefu wa mipaka. Wazir Nyalandu aliamuru mgogoro huo kumalizwa mara moja
kwa kuzingatia mipaka ya zamani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...