Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mheshimiwa, Stephen M. Wasira (Mb), ametangaza kuwasimamisha kazi watendaji watatu wa Mamlaka ya Kuendeleza Bonde la Mto Rufiji (Yaani Rufiji River Basin Development Authority – RUBADA) kutokana na tuhuma mbalimbali za ubadhirifu wa fedha za umma na matumizi mabaya ya madaraka.

Akitoa agizo hilo leo mbele ya Waandishi wa Habari, Waziri Wasira aliwataja Watendaji hao kuwa ni Bwana Aloyce L. Masanja – Kaimu Mkurugenzi Mkuu; Bibi Tabu Ndatulu – Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji; na Bwana Filozi John Mayayi – Mkurugenzi wa Fedha na Utawala.

Taarifa ya Mheshimiwa Wasira imeanisha kuwa kati ya shilingi 2.748 billion zilizokuwa zimekusanywa kwa ajili uwekezaji, ni shlingi 714.606 milioni tu ndizo zimetumika kihalali wakati kiasi kilichobaki kimetumika bila kuzingatia sheria na kanununi za fedha za umma.

Aidha, Bodi ya RUBADA imetakiwa kuteua Maafisa watakaokaimu nafasi za viongozi hao wakati mchakato wa kuwapata viongozi wa kudumu ukiendelea.

Vilevile, mamlaka zingine ikiwa ni pamoja na vyombo vya dola kama vile TAKUKURU na Polisi wanaendelea na taratibu za kuwachukulia hatua viongozi hao kwa mujibu wa sheria za nchi.
Mheshimiwa Wasira (kulia) akiongea na Waandishi wa habari (hawapo pichani). Katikati ni Katibu Mkuu Bibi Sophia Kaduma (katikati), na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Dkt. Yamungu Kayandabila.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. TAKUKURU na polisi wanaendelea na taratibu za uchunguzi na kuwachukulia hatua, pesa zimeibwa na ushahidi upo, hizo taratibu gani zingine na uchunguzi gani mwingine unahitajika? Nchi yetu ni dhaifu katika uchunguzi wa aina yoyote ndiyo maana waibaji hawaogopi.....sijawahi kuona mtu anafungwa kwa kuiba serikalini ndiyo maana wizi haukomi.

    ReplyDelete
  2. Udhaifu wa sheria ilyopo dhidi ya maadili kwa viongozi Na watumishi wa serikali ndio tatizo kubwa.nchi imejaa ufisadi kila kona.kulindana ndio sera iliyopo Na hao unaowaona wanafukuzwa Ni wachache Sana ktk mtandao mzima .mpaka Leo hii Ni aibu nchi km hii serikali kuwa Na hospitali moja Tu ya rufaa Na pesa za walipa kodi zinapotea Tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...