Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA)imeanzisha mfumo wa mafunzo stadi katika sekta ya madini na gesi ambao utasaidia watu wanaohitimu katika mafunzo hayo duniani.

Hayo ameyasema leo Mkurugenzi Mkuu wa VETA,Mhandisi Zebadiah Moshi wakati wakisaini makubaliano na serikali ya Australia kuptia shirika la Idara ya Mambo ya Nje na Biashara (DFAT)iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency,jijini Dar es Salaam.

Amesema katika makubaliano hayo,Serikali ya Australia imekubali kutoa Sh.milioni 330  kwa ajili mfumo huo ambao utatengenezwa na wataalam wa nchi hiyo.

Mhandisi Moshi amesema manufaa ya mfumo huo kwa VETA kuimarisha ushirikiano na viwanda au waajiri mbalimbali, kulenga kutoa mafunzo ambayo yanaendana na mahitaji ya soko la ajira,uboreshaji wa viwango vya mafunzo yanayotolewa na viwanda,kuipunguzia mzigo serikali katika kuilea VETA kwa kuchangia gharama za mafunzo kwa njia ya vifaa au kutoa wataalam wa kufundisha.

Naibu Waziri Mkuu wa Jimbo la Australia Magharibi na Waziri wa Afya na Utalii Dk.Kim Hemes  amesema nchi yao imepiga hatua katika utoaji wa mafunzo na viwango vyake vinatambulika duniani  katika madini,mafuta,gesi pamoja na Utalii.
Mkurugenzi wa VETA,Mhandisi Zebadiah Moshi (kushoto) akitia saini ya makubaliano kati ya Veta na Serikali ya Australia na Kulia ni Naibu Waziri Mkuu wa Jimbo la Australia Magharibi na Waziri wa Afya na Utalii Dk.Kim Hames wanaoshudia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Consolata Mgimba,Balozi wa Australia nchini,John Feakes katika hafla ya makubaliano kati ya VETA na Serikali ya Australia iliyofanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency,Jijini Dar es Salaam. 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Consolata Mgimba akizungumza na waandishi habari katika hafla ya kusaini makubaliano kati ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo Stadi (VETA),iliyofanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency,jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa VETA,Mhandisi Zebadiah Moshi na akizungumza na waandishi habari katika hafla ya kusaini makubaliano kati ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo Stadi (VETA),iliyofanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency,jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Mkuu wa Jimbo la Australia Magharibi na Waziri wa Afya na Utalii Dk.Kim Hames  akizungumza na waandishi habari katika hafla ya kusaini makubaliano kati ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo Stadi (VETA),iliyofanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency,jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Consolata Mgimba (Katikati),Kushoto ni Mkurugenzi  Mkuu wa VETA,Mhandisi Zebadiah Moshi,kulia ni Naibu Makamu,Magharibi wa Australia,Waziri wa  Afya na Utalii,Dk.Kim Hames pamoja na watendaji wa VETA na Ubalozi wakiwa katika picha ya pamoja katika hafla ya kusaini makubaliano kati ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo Stadi (VETA),iliyofanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency,jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 28, 2015

    Endelezeni taaluma na ufundi stadi katika sekta ya madini na gesi ili kuwezesha vijana wetu kuchukua ajira zitakazojitokeza.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...