Mkurugenzi  Mkuu wa  Relim Entertainment Ltd,Emelda Mwamanga akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa kuadhimisha miaka 11 ya jarida la Bang! katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dar es Salaam leo, kushoto ni Mkurugenzi wa Ubunifu na Masoko wa Relim Entertainment Ltd ,Mpegwa Mwarang’ata na Ofisa Masoko Relim Entertainment Ltd Darliana Mbedule.
 Mkurugenzi  Mkuu wa  Relim Entertainment Ltd Emelda Mwamanga wakionyesha waandishi wa habari baadhi ya habari ya Mwanawake ambaye wamemzungumzia katika la Jarida Bang! wakati wa kuadhimisha miaka 11 ya Jarida holi  leo jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi  Mkuu wa  Relim Entertainment Ltd Emelda Mwamanga akiwasha mishumaa kwenye Keki ya kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 11ya kuanzishwa kwa Jarida la  Bang! pamoja na kukata keki leo katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dar es Salaam.
  Mmiliki wa Full Shangwe blog, John Bukuku akilishwa keki na Mkurugenzi  Mkuu wa  Relim Entertainment Ltd, Emelda Mwamanga wakati wa maadhimisho ya Miaka 11 ya kuanzishwa kwa Jarida la Bang!.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
Kampuni ya Relim wachapishaji wa jarida la Bang imesema kuwa imenua wanawake wenye vipaji pamoja na kuibua vibaji kwa baadhi ya wanawake kutokana na kuandika habari zinazohusu vpaji vyao.

Akizungumza na waandishi wa habari  katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi wa Kampuni ya Relim,Emelda Mwamanga amesema katika kusherekea miaka 11 tangu kuanzishwa kwa kampuni hiyo wamefanikiwa kuinua wanawake katika sekta mbalimbali ikwemo ujasiriamali kwa kuandika habari zao na kuonekana kwa mchango wao katika jamii.

Emelda amesema jarida la Bang katika kipindi chote limekuwa likiandika habari mbalimbali katika kuinua maisha ya wanawake ,vijana na jamii katika   kutambulisha vipaji vyao.

Amesema  katika miaka 11 wamejipanga kuinua maisha ya wanawake kwa kutambulisha vipaji na biashara zao na kuandika habari mbalimbali zitakazowezesha kutambulisha Afrika yote kwa ujumla.

Emelda amesema wamekuwa wakitambua mchango wa viongozi wa siasa katika majimbo yao na kutaka katika kuelekea uchaguzi mkuu jamii iweze kuwatambua viongozi wanaowachagua kwa kuyafahamu maisha yao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...