Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambalo ni msimamizi wa sekta ya Sanaa na burudani nchini limeona picha chafu na zisizo na maadili za Msanii Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole alipokuwa akifanya onesho lake nchini Ubelgiji hivi karibuni.

Katika picha hizo ambazo zimelaaniwa na watanzania wengi nchini kupitia njia mbalimbali ikiwemo mitandao ya kijamii, Shilole anaonekana akiwa Jukwaani huku viungo vyake vya sehemu za siri vikiwa hadharani na zaidi akionesha tabia ambazo kwa kiasi kikubwa zimefedhehesha na kuidhalilisha sekta ya Sanaa na Taifa kwa ujumla.   

Aidha, BASATA limepokea malalamiko kwa njia ya simu na mawasiliano ya internet kutoka kwa watanzania waishio ughaibuni wakilaani tukio la Msanii huyo. Katika mawasiliano yao wameeleza kwamba wamefedheheshwa na kudhalilika na tabia hiyo chafu iliyooneshwa na msanii huyu.

Ikumbukwe kwamba, Shilole ni msanii aliyesajiliwa na Baraza la Sanaa la Taifa, hivyo anapokwenda nje ya nchi kabla hajapata visa anapewa barua ya utambulisho kama msanii wa Tanzania, hivyo anapokuwa nje ya nchi anatambuliwa kama msanii Mtanzania, anapofanya kinyume na misingi ya kazi ya Sanaa, anajifedhehesha yeye mwenyewe, kazi ya Sanaa na nchi yetu pia.

Aidha, ikumbukwe kwamba BASATA limeshapata kumwita na kumuonya msanii huyu kutokana na tabia yake ya kutokujiheshimu pale awapo jukwaani na yeye aliahidi kubadilika na kuachana na tabia hiyo chafu. Kwa hiyo kuendelea kwake kufanya matukio hayo na kwa sasa katika ardhi ya nchi nyingine ni uthibitisho kwamba hajabadilika na kwa maana hiyo ameendelea kuidhalilisha Sanaa na wasanii wa kitanzania wenye kujitambua na kuiheshimu Sanaa kama kazi nyingine.
BASATA linapenda kueleza kwamba;
1. Litamuita kwa mara nyingine tena kumtaka ajieleze kwa nini alifanya onesho hilo la kujidhalilisha na kudhalilisha hadhi ya mwanamke, msanii na Sanaa kwa ujumla
2. Kama maelezo yake hayataridhisha hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake maana tayari ameshadhihirisha kwamba akifanyacho si Sanaa na hakina uhusiano na kazi ya Sanaa ambayo ina heshima yake na inahitaji ubunifu, weledi na kujitambua.

BASATA linawakumbusha wasanii wote nchini kuwa Sanaa ni kazi kama kazi zingine lakini siku za hivi karibuni wasanii wengi wamekuwa wakikiuka suala zima la maadili kwa kutengeneza kazi chafu zisizofaa mbele ya jamii ya watanzania wanaoipenda na kuiheshimu kazi ya Sanaa yenye staha. Tuungane kwa pamoja kukemea kazi chafu zinazozalishwa na wasanii wasiojitambua kwani suala la maadili ni suala mtambuka na linaanzia katika ngazi ya familia. 

Aidha, BASATA linawataka Wasanii wote nchini kufuata sheria, kanuni na taratibu mara wanapopata mialiko ya kikazi kwenda nje ya nchi. Linawakumbusha kwamba haiwezekani msanii kutumia picha chafu na mavazi dhalili na kuonyesha utupu katika kuvuta mashabiki.

Sanaa ni kazi, tuipende na kuithamini

Godfrey Mngereza
KATIBU MTENDAJI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 14, 2015

    acheni wivu, huko ni ulaya bwana wamezoea vitu kama hivyo.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 14, 2015

    Kweli? Hii ya ni karne:( Hivi mmekosa ya kufanya? Mbona wasanii wanalilia Hati miliki za kazi zao kila uchao na hatujawasikia wakiitisha serikali...mnafahamu sheria? Au mnahitaji shule? Mbona hamkumuita Masogange? Ikumbukwe alikamatwa S.Africa na madawa.. nani anawapa nguvu hizi za kisheria kama siyo ubabe? Taifa lina kazi kubwa ya kutooomeza umasikini ujinga na maradhi ndiyo kazi ya serikali siyo kuhangaika na akifanyacho Shilole tena Ubelgiji wala siyo kariakoo..kwa nini asikamatwe huko Ubelgiji? Wenzetu wameendelea kwa kuwekeza kwenye mambo yenye tija siyo kutumia nguvu za serikali kuwadhalilisha raia..Alichokifanya Ubelgiji wewe kinakukuna nini? Kama ni mila na desturi mngeanza kwa Mahoteli na nyumba za Wageni zinazoruhusu michepuko mbona hatuwasikii mkiitisha sheria za vyeti vya ndoa huko mahotelini? Nchi inaangamia kwa maambukizi ya ukimwi:( mfikiri kabla ya kukurupuka.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 14, 2015

    eti baraza la usanii la taifa! Hebu tafuteni vitu vya maana vya kufanya badala ya kusakama watu.Kwanza mna hakika na hicho kilichotokea? Au mnakurupuka?

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 14, 2015

    Anko hili balaza sindio linahusika pia na lugha yetu ya Kiswahili si ndio hili kama sijakosea anko ?
    Msijifanye kutoa macho saana katika swala la Shilole wakati Shilole mwenyewe kapinda kitambo ! Kuna mambo ya maana sana hamtaki hata kuyafwatila ! Mfano watu wanaofunga ndoa nje ya nchi baada ya taratibu zote kukamilika kuna karatasi unatakiwa urudishe RITA , RITA wanakuambia ndoa yako tutaisajili baada ya hicho cheti chako chandoa kilicho toka ugaibuni kwenda kutafsiliwa na wataalamu wanao tambulika na BASATA. Hapo ndio ninapowaona hawa BASATA hawajitambui . Unakwenda ofisini kwao watakacho kueleza wala hutakielewa , watakupa namba za simu za hao wataalamu wa kutafsiri lugha , namba zote utapiga hazipokelewi sijui ni kanjanja au vipi ! Mwisho unazifungia tu hizokaratasi kabatini ,mpaka hapo hao BASATA watakapo fufuka ! Leo wanajifanya wako makini kwa swala la Shilole tu ! Acheni utani tafadhali ! Kunamambo mengi sana yamaana mmekaa kimya tu !

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 14, 2015

    KWA KUFUATILIA VITU VIDOGO VINAVYOHUSU MAISHA BINAFSI YA WATU HAMJAMBO ILA KWA KUFUATILIA MAMBO YANAYOATHIRI MAISHA YA WATU WENGI KAMA UFISADI, UZEMBE KAZINI, WIZI, UBADHIRIFU WA FEDHA ZA UMMA,MAUAJI YA ALBINO NA UTOROSHAJI NA MAUAJI YA TEMBO MNALALA USINGIZI MZITO. KWANI SUALA LA SHILOLE KUACHIA MAZIWA YAKE KUNA SHIDA GANI???? MBONA HAMUWAKAMATI WABARBAIG, WAMASAI NA WENGINEO WANAOACHIA MAZIWA YAO WAZI?? MBONA SITTI HAMKUMUADHIBU WAKATI AMEDANGANYA NA KUFOJI VITAMBULISHO LICHA YA KURUDISHA MIAKA NYUMA? ACHENI SIJUI BARAZA LA NINI VILE KU-CONTROL MAISHA YA WATU BINAFSI.KAMA AMEIBIKA AMEAIBIKA MWENYEWE NA MAZIWA YAKE......TAIFA HALINA MAZIWA NA LITABAKIA TAIFA WALA HALITAABIKA LOLOTE. TUNA TATIZO LA VIONGOZI WENYE KUFANYA KAZI KAMA ZIMAMOTO WANASUBIRI LITOKEE JAMBO HALAFU MARA MOJA WALIRUKIE KUONYESHA WANAFANYA KAZI.KUNA MAMBO MENGI YA MSINGI NINYI WIZARA HAMJAFANYA HADI LEO, KAZI YENU KUKIMBILIA ADHABU ZISIZO NA MAANA. SHILOLE ANA UHURU WA KUFANYA ANALOONA LINAMFAA....MBONA HAJAKAMATWA HUKO ALIKOFANYIA HAYO???

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 14, 2015

    Basata huo sasa wivu, mbona mashindano ya ma miss hamkuona hayo mambo watu walikuwa wanakaa utupu na vinguo vya kuogelea mbona hamja kemea.
    Huo ni uonevu, mmemuona Shilole tu, je vipi vigodoro?

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 14, 2015

    Huyu amezidi kuonesha utupu wake. Afungiwe huyu. Anatumia mwili kuvuta wateja zaidi ya ujuzi wa kimziki.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 14, 2015

    Godfrey Mngereza naona hauna kazi ya kufanya! tukio limefanywa nje ya Tanzania wewe unataka kuwaonesha watanzania kwamba unajua sheria na Kazi sana si ndio??...Get a life please na kamuulize Janet Jackson kwanini alivua sidiria na kuweka wazi maziwa yake kwenye Super Bowl na kwanini Madonna (miaka 56) alimkiss Drake (miaka 28) kwenye Coachella.

    So hiyo ni art so u do everything and anything to please your fans. hope u now understand it

    ReplyDelete
  9. WILSON MARTINA GALASIANMay 14, 2015

    KAKA ISSA MAONI YOTE YANAPINGA KITENDO CHA KUTAKA KUMFUATILIA MAISHA YA HUYO MDADA HATA AKITEMBEA UCHI SISI YANATUUHUSU NINI MWENYEWE NA WAZAZI WAKE ETI TAIFA LINAHAIBIKA MBONA MASHINDANO YA WADADA ETI NDO MAMISS WANATEMBEA NA VICHUPI SEMBUSE HUYO TENA YUKO NG'AMBO EMBU WAMBIE SIE HATUJAHAIBIKA NA LOLOTE, WAMUACHE NA MAISHA YAKE EBOO!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...