Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB,Bw.Edmund Mkwawa akipokea cheti cha kutambulika katika mafunzo ya Ukurugenzi wa benki hiyo. 
 Meneja Masoko wa benki ya DCB,Boyd Mwaisame(kulia) akipokea cheti cha utumishi wa muda mrefu na maendeleo ya benki ya DCB kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Mhe.Raymond Mushi.
 Baadhi ya wadau na wafanyakazi wa benki ya DCB wakiserebuka kwa pamoja katika hafla ya kukabidhi zawadi ya Mwenyekiti wa Bodi ya DCB kwa Tawi lililofanya vizuri kwa mwezi Julai hadi Desemba mwaka 2014.
  
Na Bakari Issa.

Wanahisa na wadau mbalimbali wametakiwa kuitumia kikamilifu benki ya DCB ili kuiwezesha kutimiza malengo ya kuanzishwa kwa benki hiyo.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Mhe.Raymond Mushi katika hafla ya kukabidhi zawadi ya Mwenyekiti wa Bodi ya DCB kwa Tawi lililofanya vizuri kwa mwezi Julai hadi Desemba mwaka 2014.

Katika hafla hiyo,Mhe.Mushi ameisifu benki hiyo ya DCB kutoa huduma zake kwa njia ya kisasa(Mtandao wa Intaneti) na kusema kuwa ni benki ambayo huduma zake ndiyo silaha kubwa katika ushindani wa mabenki.

Pia,amewahimiza wafanyakazi na matawi ya benki hiyo kufanya kazi kwa ari na nguvu mpya ili waweze kufanya vizuri ili baadae wapate zawadi kama wafanyakazi wa tawi la Ukonga walioshika nafasi ya kwanza kwa asilimia 80 kwa mwaka 2014.

Kwa upande wake,Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo,Bw.Edmund Mkwawa amesema benki imepata faida ya Sh.3.7Bilioni kwa mwaka 2013 kutokana na ongezeko la matawi kama tawi la Kariakoo,Mabibo na Chanika.

Hata hivyo,Mkwawa ameyataja matarajio ya benki hiyo kwa mwaka 2015,kuwa ni kuongeza amana kwa (33%),kuongeza mikopo kwa wateja pamoja na kutoa huduma bora naza haraka zaidi kwa wateja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...