Ripoti kutoka Bujumbura, nchini Burundi zinasema kuwa kamanda mmoja wa kijeshi ametangaza kuwa hamtambui tena Pierre Nkurunziza kama rais wa Burundi.

Meja Jenerali Godefroid Niyombareh amewaambia waandishi wa habari mjini Bujumubura, kuwa kumeundwa kamati maalum ya kuiokoa Burundi itakayotawala taifa hilo kwa kipindi cha mpwito.

Kulingana na taarifa iliyopeperushwa na redio Isanganiro, serikali ya Nkurunziza imeon'golewa madarakani.

Meja Generali Niyombareh amesema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza.

Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari anasema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa.

Kwa sasa rais Nkurunziza yuko nchini Tanzania alipokuwa anatarajiwa kujumuika na viongozi wa kanda hii ya Afrika Mashriki kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu.

Jenerali Niyombareh alikuwa ameandamana na viongozi wengine wa jeshi la Burundi.

Tayari wanajeshi wameshika doria nje ya makao makuu ya runinga ya taifa.

Rais Nkurunzinza alikuwa amepuzilia mbali maombi ya kuahirisha uchaguzi huo.

Duru kutoka Burundi zinasema kuwa raia wameshajitokeza mabarabarani wakishangilia kauli hiyo ya ''Mapinduzi''.

CHANZO: BBC SWAHILI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 13, 2015

    Saaaaaaaaaaaaaafi sana kuona kwamba huyu jamaa ameondoka madarakani, niliwaambia kabisa mapema hapa hapa kwamba tusilete mazungumzo na mtu ambae hataki kuheshimu demokrasia na katiba ya nchi yake! Kumng'oa madarakani ndio suluhisho pekee.

    Kinachohitajika sasa ni kuwapatia nguvu hawa askari walio mpindua ili wasije wakazidiwa nguvu na askari ambao watakuwa bado wanamfuata Pierre Nkurunziza na kufanikisha kurudi madarakani.

    Vile vile hawa askari wawekewe mkakati wa wazi wazi kabisa kwamba ni lini (time frame) watarudisha Serikali ya kidemokrasia na ya watu ili wasije wakaingiwa na tamaa ya kubaki madarakani. Tanzania au EAC kwa ujumla na AU wanaweza wakahusika hapa.

    Vile vile hawa askari wasije wakavunja haki zozote za binadamu au kufuja resources za Burundi.

    Pongezi kwa wote waliohusika kushawishi Jeshi la Burundi kufanya mapinduzi na haswa haswa kumshawishi Major General Godefroid Niyombare kufanya mapinduzi ya msingi kuokoa Taifa la Burundi maana maamuzi haya yataifanya nchi yetu Tanzania kuwa katika Mazingira yaliyo salama.

    Hii iwe fundisho kwa Viongozi wote wa Afrika wanaopenda kuvunja demokrasia au Katiba ya nchi zao.

    Asante.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 13, 2015

    Burundi isuluhishe matatizo yake kwa amani.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 13, 2015

    Ndugu zangu watanzania mkaangalie video you tube ya mwalimu julius nyerere .Alisema hivi vinchi vidogividogo vitatumika na wabepari kwa manufaa Yao .Wataanzisha vuruguvurugu ili wawape masharti makali kuwasaidia.Obama ni raisi wa USA ambae kwenye uongozi wake kumetokea vuruguvurugu mno kila kona na wanaangalia tu .Sasa sisi watanzania tuwe macho mnoooo.Kuna scandals hapa USA ya Bill clinton foundation baada ya scandal kuvuja bill clinton a kaenda Tanzania juzijuzi tu .Na Unaambiwa kukiwa na crisis bill clinton foundation wanakuwa wa kwanza kuwasili na hakuna wanachofanya zaidi .Tuwe macho sana na hawa watu na hizi vuruguvurugu

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 13, 2015

    Kama kijana huyu ana akili basi atawachia ngazi muda wake ukifika

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 14, 2015

    Afrika tuna matatizo. Kama muda wa kutawala umeisha kwa nini usiondoke ukawapisha wengine. Angalia wananchi wako wanavyoteseka hasa wanawake na watoto.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...