Meneja
Biashara wa Idara ya Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Grace
Lyon akiwapa elimu kuhusiana na matumizi ya vitambaa vya hedhi baadhi
ya wanafunzi wa shule ya msingi iliyopo
Hydom Mkoa wa Manyara.Vodacom Foundation kupitia mradi wake wa Girl
Pawa imelenga kuwawezesha wasichana kutimiza ndoto za maisha yao kwa
kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowafanya wasibaki nyuma
katika masomo, kutojiamini na utoro mashuleni wanapokuwa
kwenye vipindi vya hedhi.Mradi huu ambao unatekelezwa na taasisi ya
T-MARC wakishirikiana na USAID pamoja na
Vodacom Foundation leo zimeungana na mataifa mengine katika kuadhimisha siku ya hedhi duniani.
Changamoto
mbalimbali zinazowakabili wasichana wanapokuwa kwenye vipindi vya hedhi
yanapaswa kujadiliwa na kutafutiwa ufumbuzi wa kudumu kwa kuwa
yanachangia
kurudisha nyuma jitihada za kuwainua watoto wa kike nchini.
Wito
huo umetolewa na Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania
Rosalynn Mworia ikiwa leo ni maadhimisho ya siku ya hedhi duniani ambapo
Vodacom Foundation, imekuwa mstari
wa mbele kupambana na changamoto zinazowakabili watoto wa kike nchini
ikiwemo kusaidia wasichana vifaa vya kuwaweka salama wanapokuwa kwenye
vipindi vya hedhi kupitia mradi wake wa
Girl Pawa wenye kauli mbiu isemayo “Hakuna Wasichoweza”.
“Vodacom
Foundation kupitia mradi wake wa Girl Pawa imelenga kuwawezesha
wasichana kutimiza ndoto za maisha yao kwa kukabiliana na changamoto
mbalimbali zinazowafanya wabaki
nyuma baadhi yake zikiwa ni ukosefu wa elimu , kutojiamini na utoro
mashuleni wanapokuwa kwenye vipindi vya hedhi.Mradi huu ambao
unatekelezwa na taasisi ya T-MARC umeonyesha mafanikio katika awamu ya
kwanza.”Alisema.
Mworia alisema lengo la mradi wa “Hakuna Wasichoweza”
ni kuwapatia elimu ya uzazi, afya, kuwajengea uwezo wa kujiamini na
kuwapatia Pedi za gharama nafuu watoto
wa kike waliopo katika umri wa kuvunja ungo na umeanza kutekelezwa
mkoani Mtwara lengo likiwa ni kutekelezwa katika mikoa mbalimbali ya
Tanzania katika siku za usoni.
Meneja wa mradi huu wa T-MARC,Doris Chalambo amesema tangu mradi huu uanze kutekelezwa
idadi ya wasichana
wanaohudhuria masomo mashuleni imeongezeka tofauti na siku za nyuma
ambapo wasichana walipokuwa wanaingia katika hedhi wengi wao walikuwa
wanashindwa kuhudhuria kwenye masomo kutokana na kutokuwepo
na mazingira rafiki ya kukabiliana na hali hiyo
Kutokana na mafanikio yaliyopatikana katika awamu ya kwanza ya mradi wa kuwawezesha wasichana kupitia mradi wa
Hakuna Wasichoweza, taasisi ya Vodacom Foundation imeongeza
ufadhili wa Dola za Kimarekani 166,000 katika awamu ya pili ili mradi
uendelee na uweze kuwafikia wasichana wengine wapatao 4,200 katika shule
nyingine 10 katika mkoa wa Mtwara.
Awamu
ya kwanza ya mradi huu ilifadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Watu wa
Marekani (USAID) ambalo lilitoa ufadhili wa Dola za Kimarekani 200,000
na taasisi ya Vodacom
Foundation ambayo ilitoa Dola za Kimarekani 100,000 na umenufaisha
zaidi ya wasichana 5,000 ambapo katika awamu ya pili unategemewa
kunufaisha wasichana wengi zaidi.
Serikali
nayo imetangaza kulivalia njuga tatizo hili ambapo hivi karibuni
imesema kuwa itaboresha mazingira kwenye shule zake ili yawe rafiki kwa
wasichana wanapokuwa
kwenye hedhi ili kupunguza utoro mashuleni.Kauli mbiu ya siku ya hedhi
duniani mwaka huu ni “Usisite Kuzungumzia Hedhi”.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...