Mwenyekiti wa Posta
na Simu SACCOS, Bw. Lawrence Mwasikili (katikati) akisisitiza jambo wakati
alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuanza kuuzwa kwa viwanja 1,500
vilivyoko Msata, wilaya ya Bagamoyo kwa wanachama wake. Walioambatana naye katika mkutano huo wa
waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam ni Afisa Mkuu Mtendaji wa
Ushirika huo, Bw. Deogratias Ngalawa (kushoto) na Afisa Tawala, Bw. Jeremiah
Miselya.
Afisa Mkuu
Mtendaji wa Posta na Simu SACCOS, Bw. Deogratias Ngalawa akisisitiza jambo
wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuanza kuuzwa kwa
viwanja 1,500 vilivyoko Msata, wilaya ya Bagamoyo kwa wanachama wake. Wengine walioambatana naye katika mkutano huo
wa waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam ni Mwenyekiti wa Ushirika huo,
Bw. Lawrence Mwasikili (katikati) na Afisa Tawala, Bw. Jeremiah Miselya
(kulia).
Posta na Simu Saccos Ltd imewaalika wanachama wake kununua viwanja vilivyopimwa Msata, wilaya ya Bagamoyo kuanzia jana hadi tarehe 31 Mei, 2015 ili wajenge nyumba bora au watume hati za viwanja kupata mikopo mikubwa.
Akitangaza uamuzi
wa ushirika huu jana Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wake, Bw Lawrence
Mwasikili, amesema kuwa viwanja viko katika makundi matatu na bei zake ni
tofauti. Viwanja vya maeneo madogo ni
870 na kila kiwanja kinagharimu milioni 2; ukubwa wa kati ni viwanja 465 na
kiwanja kitapatikana kwa milioni 3.5.
Viwanja ya maeneo makubwa ni 165 na kila kiwanja ni milioni 5.
Amesema kuwa kwa
wanachama fedha ya kumilikishwa viwanja
itakatwa kwenye mishahara yao kwa miaka miwili.
Bw Mwasikili
amewahakikishia wanachama kuwa upimaji wa viwanja hivyo umethibitishwa na
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, na kueleza kuwa wanachama
lazima waombe umiliki wa viwanja hivyo katika kipindi kilichowekwa kwani baada
ya 31 Mei, 2015, watu wasiokuwa wanachama wataalikwa kumiliki viwanja hivyo kwa
utaratibu kununua mita ya mraba kwa shilingi 4,500.
Amesema kuwa
uamuzi huu unatokana na ukweli kwamba wanachama wa ushirika huu wengi wana
nyumba katika maeneo yasiyopimwa na kwa hiyo hawawezi kupata mikopo.
Akisisitiza umuhimu wa wanachama kuchukua
viwanja kwa utaratibu wa upendeleo katika muda
uliotengwa, Mwenyekiti alisema “tutawaalika wananchi wa kawaida kuchukua
viwanja hivi kuanzia Juni mosi, mwaka huu.” Wananchi wapata viwanja kwa kulipa fedha taslimu mara
moja au kwa mikupuo itakayoidhinishwa.
Katika mkutano
huo, Ofisa Mkuu (CEO)wa ushirika huu,Bw. Deogratias Ngalawa, aliwambia
waandishi wa habari kuwa wanachama
wachangamkie fursa hiyo kwa vile viwanja
vitapatikana kwa gharama ndogo
ikilinganishwa na gharama za viwanja vilivyopimwa vya taasisi nyingine.
Alisema ushirika
wao umkopesha mwanachama hdi milioni 25 na kwa kuwa kuna wanachama wanohitaji
mikopo mikubwa hati za viwanja hivi zitawasaidia kupata mikopo watakayoomba.
Wanachama wa
Posta na Simu Saccos ni wafanyakazi
wa Shirika la Posta Tanzania,
Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Tanzania Postal Bank (TPB) na Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCCRA).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...