Watu wapatao 12 wamethibitishwa kupoteza maisha jijini Dar es Salaam kutokana na athari za mafuriko kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha katika jiji hilo. 

Idadi hii inatokana na taarifa ya awali ya Jeshi la Polisi kwa vyombo vya habari iliyotaja idadi ya waliopoteza maisha kuwa ni wanane (08). Hili ni ongezeko zaidi ya watu waanne (04). Watu walioripotiwa kuongezeka hadi sasa ni kama ifuatavyo:

1. Mnamo 09/05/2015 majira ya saa 12:00 katika bonde la mto Mkwajuni, mtaa wa Makuti, Magomeni wilaya ya Kinondoni, ulipatikana mwili wa mtu mmoja mwanamke anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 40 – 45 akiwa amefariki dunia. Mwanamke huyu ambaye hakufahamika jina, umri, wala makazi yake  alikuwa amevalia nguo aina ya dera rangi ya njano. Mwili mehifadhiwa katika hospitali ya muhimbili kwa utambuzi.

2. Mtu mwingine VALERIAN S/O ERADIUS, Miaka 13, Mwanafunzi wa kidato cha kwanza, shule ya sekondari Kigogo, Mkazi wa Mburahati kwa Shebe amefariki dunia tarehe 10/05/2015 baada ya kuangukiwa na ukuta kufuatia mvua kunyesha jijini Dar es Salaam. Mwili umehifadhiwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili.

3. Mnamo tarehe 08/05/2015 huko maeneo ya Mbezi Beach Kilongamiwa Tarafa ya Kawe wilaya ya Kinondoni mtu mmoja  aitwaye GERVAS S/O  SHAYO, Miaka 28, shamba boy,  mkazi wa Mbezi juu alikuwa amekufa maji. Mtoa taarifa PROCHES S/O SEBASTIAN, Miaka 34, Mkazi wa Mbezi beach alisema taarifa toka kwa mke wa marehemu zinasema siku ya tukio marehemu alisikika akiomba msaada wa kuvushwa mtu huona baadaye hakurudi nyumbani hadi alipogundulika akiwa amefariki dunia. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala kwa uchunguzi.

4. Mtu mwingine mwanaume anayekadiriwa kuwa naumsri kati ya miaka (35 – 38) ambaye jina, umri wala makazi yake hayajajulikana mara moja ameopolewa katika tope leo tarehe 11/05/2015 maeneo ya Magomeni Suna katika bonde la Mto Msimbazi akiwa tayari ameshafariki dunia. Mwili wake umehifadhiwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa uchunguzi na utambuzi
Aidha, uzoefu unaonyesha kuwa jinsi maji yanavyoendelea kupungua kutokana na kupungua kwa mvua ndo madhara yanavyoendelea kuonekana. 

Nawataka wananchi waendelee kutoa taarifa za mapema ili hatua zichukuliwe mara moja ikiwa ni pamoja na kuiondoa miili ya watu watakaokuwa wamepoteza maisha kutokana na athari za mvua zinazoendelea kunyesha katika jiji la Dar es Salaam.

Wananchi wanaombwa kuzingatia taarifa zinazotolewa na mamlaka ya hali ya hewa kuhusu hali ya hewa nchini ili wawe katika hali ya tahadhali ili kupunguza madhara yanayoweza kutokea.

S. H. KOVA
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...