Mkurugenzi Idara ya Uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig.Jen. Mbazi Msuya akimpongeza Nahodha wa meli ya Mv. Liemba, Mande Mangapi mara baada ya kuwafikisha salama waomba hifadhi ya ukimbizi kutoka Burundi wapatao 600, katika bandari ya Kigoma kutoka Kagunga, saa mbili usiku tarehe 15 Mei 2015, kushoto ni Kaimu Katibu Tawala mkoani Kigoma, Salvatory Shauri.
Ujumbe uliongozwa na Mkurugenzi Idara ya Uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig.Jen. Mbazi Msuya ukiwa katika bandari ya Kigoma kwa ajili ya kuwapokea waomba hifadhi ya ukimbizi kutoka Burundi mara baada ya kuwasili kutoka kijiji cha Kagunga na Meli ya Mv. Liemba saa mbili usiku, tarehe 15 Mei 2015.
Baadhi ya waomba hifadhi ya ukimbizi kutoka Burundi wakiwasili katika bandari ya Kigoma kutoka kijiji cha Kagunga na Meli ya Mv. Liemba saa mbili usiku, tarehe 15 Mei 2015.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...