Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi akitoa hotuba kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe kushukuru msaada wa mashine zilizotolewa na Serikali ya Marekani kwa Jeshi la Polisi Tanzania kwa ajili ya kuweka alama silaha.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IJP Ernest Mangu akishukuru kuhusu msaada wa mashine za kuweka alama silaha zilizotolewa na Serikali ya Marekani kwa Jeshi la Polisi Tanzania katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi jijini Dar es Salaam. Waliokaa toka kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi na Katibu Mtendaji wa Kituo cha Kikanda cha kushughulikia Silaha Ndogondogo, Bw. Theoneste Mutsindashyaka.
Katibu Mtendaji wa Kituo cha Kikanda cha kushughulikia Silaha Ndogondogo (RESCA), Bw. Theoneste Mutsindashyaka (kulia) akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi, mashine 2 za kuweka alama silaha, zilizotolewa na Serikali ya Marekani kupitia Kituo hicho chenye Makao Makuu yake Jijini Nairobi. Halfa hii ilifanyika katika Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...