Majenerali wawili waliotekeleza jaribio la mapinduzi nchini Burundi dhidi ya rais Pierre Nkurunziza wametiwa mbaroni baada kushidwa kwa jaribio lao hilo, huku kiongozi mkuu wa mapinduzi hayo jenerali Godefroid Niyombare akidaiwa kuingia mititi na sasa anasakwa.
Hayo yemeelezwa leo hii na Msemaji wa Rais Nkurunziza,Willy Nyamitwe.
Awali Jenerali Niyombare alikaririwa akikiambia chombo cha habari cha AFP kwamba yeye na wafuasi wake watajisalimisha kwa serikali ya Rais Nkurunziza, huku akiongezea kuwa ''natumai hawatatuua''.
![]() |
Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza |
Naibu kiongozi wa jaribio la mapinduzi nchini Burundi, alikiri kuwa jaribio lao limeshindwa kufanikiwa, baada ya kukabiliana na upinzani mkali kutoka kwa jeshi la taifa hilo. Habari za kushindwa huko zimetolewa wakati rais Pierre Nkurunziza akitangaza kuwa amerejea nchini Burundi.
Akitangaza kupitia ukurasa wake wa Twitter, Nkurunziza aliwashukuru wanajeshi na polisi kwa ''uzalendo wao'', na wananchi wa Burundi kwa ''subira'' waliyoidhihirisha.
Majaribio ya kuiangusha serikali ya rais Pierre Nkurunziza yalitokea yeye akiwa nchini Tanzania, alikokuwa amekwenda kuhudhuria mkutano wa marais wa kikanda kuhusu hali ya kisiasa nchini mwake.
![]() |
Kiongozi mkuu wa Jaribio la Mapindizi nchini Burundi,Meja Jenerali Godifroid Niyombare |
Lakini mpaka wakati huu, haijulikani hasa wapi alipo rais huyo, na taarifa za kurejea kwake hazikuthibitishwa na vyanzo huru.
Kufuatia mkutano wa dharura jana Alhamisi, Baraza la amani na usalama la Umoja wa Afrika, lililaani jaribio lolote la kutwaa madaraka kupitia vurugu nchini Burundi, na kuhimiza mazungumzo kati ya makundi yanayohasimiana.
Mjini New York, Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon na maafisa wake waandamizi, walikuwa wanafuatilia matukio nchini Burundi kwa wasiwasi mkubwa, alisema msemaji wake.
Nalo Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeonya kuwa litawachukulia hatua wale wote wanaowafanyia vurugu raia na kutaka kurejeshwa haraka kwa utawala wa sheria.
Hii ni hatua nzuri, hakuna sababu ya vita wala wananchi kuuana Burundi. Waliosababisha jaribio la mapinduzi wajibu mashitaka kwa mujibu wa sheria, Burundi ikae kwa amani na utengamano. Funzo ni vijana wacha kushabikia vita yoyote inaahthiri sio nzuri.
ReplyDelete