Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe (kushoto), akizungumza na Kamishna wa Forodha na Ulinzi wa Mipaka toka Serikali ya Marekani Bw. R. Gil Kerlikowske alipomtembelea ofisini kwake kuzungumzia masuala ya ushirikiano wa shughuli za kiulinzi kati ya Serikali ya Tanzania na Marekani. Kulia ni Msaidizi wa Balozi wa Marekani hapa nchini Bi. Virginia Blaser.
Kamishna wa Forodha na Ulinzi wa Mipaka toka Serikali ya Marekani Bw. R. Gil Kerlikowske (kulia), akifafanua jambo kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe wakati wa mazungumzo yaliyofanyika Ofisini kwa Waziri Chikawe kuhusu kuimarisha ushirikiano wa masuala ya kiulinzi kati ya Serikali ya Tanzania na Marekani.
Ujumbe kutoka Serikali ya Marekani wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mathias Chikawe alipokuwa akizungumza nao wakati walipotembelea Ofisini kwa Waziri Chikawe. Ujumbe huo uliongozana na Kamishna wa Forodha na Ulinzi wa Mipaka toka Serikali ya Marekani Bw. R. Gil Kerlikowske.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mathias Chikawe (kulia), akizungumza na Kamishna wa Forodha na Ulinzi wa Mipaka toka Serikali ya Marekani Bw. R.Gil Kerlikowske (katikati) wakati akiondoka mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ofisini kwa Waziri Chikawe. Kushoto ni Msaidizi wa Balozi wa Marekani hapa nchini Bi. Virginia Blaser.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...