Huu si Mto lakini ni Maji Machafu ambayo yamefumuka kwenye Chemba baada ya Mvua kunyesha Katika mtaa wa Nzasa zamani Umoja Street Mwenge ambao pia unajulikana kama mtaa wa Kinyesi
Haya ni maji machafu ambayo yanatoka katika Chemba za maji taka ambapo yanapita kando ya makazi ya watu na kusababisha Kero ya Harufu mbaya na wasiwasi wa Mlipuko wa Magonjwa.
Hii ni Moja ya Chemba ikiwa inafuka Maji Machafu ambayo yamejitengenezea Njia katika Makazi ya watu
Na hii pia ni Chemba ambayo imefumuka na Kusababisha matatizo katika mtaa wa Nzasa Mwenge
Hivi huko Dawasco kuna wataalam kweli au ndo wataalam wa makaratasi!
ReplyDeletehivi hapa kuna viongozi kweli? Viongozi wa Serikali ya mtaa na halmashauri kwanini wasifanye kazi? kama kunavijana ambao hawana ajira kwannini serikali ya mtaa isiorganize watu wachangie hasa wenye nyumba na wapangaji wao ili wa rekebishe? hizi nyumba watu watakipaje property tax kwa huduma kama hizi? nadhani viongozi tunaowachagua tusiwachague kwa ushcbiki wa kichama bali kwa ambayo watakayoweza kutufanyia.
ReplyDeleteMwaka 2005 ama 2007 wachina wlikuwa wanabadilisha mabomba ya maji machafu hayo. Kilichofanyika kilikuwa ni kichekesho waliondoa mabomba yenye kipenyo kikubwa wakarudisha yale yenye kipenyo kidogo.
ReplyDeleteNilimwendea msimamizi mmoja ambaye ni mtanzania na kumuuliza kulikoni wanafanya hivyo, akajibu eti wanayoweka yana ubora kwani yanateleza na hivyo kupelekea maji machafu kupita kwa kasi. Nikachoka nikaondoka, hata hivyo muziki huo ni wa kawaida tokea miaka hiyo, masika ikiisha kunakuwa na mbu tani mia moja.
Haya taasisi husika usingoje taarifa nyingine rekebisha hili tatizo. Kazi ya kuweka upya bomba la maji machafu la jiji la Dar-es-Salaam isichelewe la sivyo hali ya afya za watu iko hatarini. Katika mpango wa maendeleo ujao uwepo mkakati wa kupanua sehemu zinazohitaji huduma hii, hasa wale wenye water table za juu, wote wanahitaji centralized sewage system inayokidhi haja.
ReplyDeleteTunahitaji kodi maalumu kuchangia uwekezaji katika miundo mbinu hii.
ReplyDeleteHakuna usanifu unaoweza kukidhi kupitisha takataka ngumu kama viroba,chupa za maji na matambara kwenye bomba hizo. Kubadili tabia zetu ndio suluhu kubwa ya matatizo yetu badala ya lawama zisizo na tija.
ReplyDeletehalafu bado mtu akisema anauza nyumba maeneo haya ni sawa na bei ya kununulia ndege..... maradhi matupu. mweeeh! bado ntabakia huku kwenye nafasi na hewa nzuri
ReplyDeleteDar imeshindikana wadau hata wataalamu.wamechoka kufikiri
ReplyDeleteKila mtu anapaswa kuwajibika katika nafasi alionayo. Huwezi kumlaumu mwenyekiti wa mtaa wakati wewe mwenyewe ndie unaetupa uchafu usiostahiki katika mtaro. Huyo ambae yupo karibu na hiyo chemba amewajibika kwa kiwango kipi hadi hali inafikia kuwa hapo ilipo????
ReplyDeleteInasikitisha kwamba hii ni tatizo ambalo linajulikana kwa muda mrefu, na katika wataalam wote tulio nao, wanashindwa kulifanyia kazi.
ReplyDeleteHali kama hii inaongeza kero kwa wakazi na gharama kwa wananchi maana ni wazi magojwa mlipuko yanatokea sana kwenye hizi hali.