Mkuu wa mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya (mwenye koti) akipata maelezo ya njia ya kutembea kwa miguu kutoka Kagunga hadi Mkigo kutoka kwa mkazi wa kijiji hicho, Mahmud Ahmad wakati alipokagua njia hiyo ili itumike kuwasafirisha waomba hifadhi ya ukimbizi wa Burundi, tarehe 17 Mei, 2015, (mwenye Kaunda suti ) ni Mkurugenzi Idara ya uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig.Jen, Mbazi Msuya.
Mkuu wa mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya (mwenye koti) akiwa katika kijiji cha Kilemba kwa ajili ya kuwapokea waomba hifadhi ya ukimbizi wa Burundi waliokuwa wanasafirishwa kwa kutembea kwa miguu kutoka kijiji cha kagunga hadi kijijini hapo ili wapelekwe kambini (mwenye Kaunda suti ) ni Mkurugenzi Idara ya uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig.Jen, Mbazi Msuya, Mkuu wa Kikosi cha Jeshi la Wananchi 24 KJ Kigoma, Luteni Kanali Donald Msengi (katikati) na Kaimu Katibu tawala wa mkoa wa Kigoma, Salvatory Shauri tarehe 17 Mei, 2015.
Mkuu wa mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya akiongea na vijana ambao ni waomba hifadhi ya ukimbizi kutoka Burundi mara baada ya kuwapokea vijana hao walipofika kijijini Kilemba ili wapelekwe kambini baada ya kusafirishwa kwa kutembea kwa miguu kutoka kijiji cha kagunga tarehe 17 Mei, 2015.
Baadhi ya vijana takribani 36 ambao ni waomba hifadhi ya ukimbizi kutoka Burundi wakiwa wamepunzika kijiini Kilemba kabla ya kusafirishwa na basi kwenda kwenye kambini mara baada ya kusafirishwa kwa kutembea kwa miguu kutoka kijiji cha kagunga tarehe 17 Mei, 2015.
Mkurugenzi Idara ya uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig.Jen, Mbazi Msuya akiongea na mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la kusafirisha wakimbizi, Son Ha Dinh, mara baada ya kuwasafirisha vijana takribani 36 ambao ni waomba hifadhi ya ukimbizi kutoka Burundi kutoka kijiji cha kagunga, tarehe 17 Mei, 2015.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 20, 2015

    Hizi pongezi za kutubuniwa tu. Lini nchi yetu na viongozi wake wataamka? Hawa pia tutawapa uraia?

    Sisi mkoani Kigoma na Sumbawanga tunaona maslahi ya watu wa nchi nyingine yanapewa kipaumbele kuliko ya kwetu.

    Ni hivi karibuni tu tumewapa uraia watu laki mbili. Si ajabu kwamba wengine wanaona hii in njia mbadala ya kupata fursa kama hiyo pia.

    Hao wanaotupongeza kwao hawachukui watu lukuki kama tufanyavyo. Viongozi wasituharibie nchi yetu.

    Walipo wakimbizi waliopewa uraia in wengi kuliko wenyeji. Sasa hilo in kabila lingine tumeanzisha ama kitu gani. Na wabunge wetu wamenyamaza tu.

    Tunataka viongozi wanao simamia maslahi yetu kwanza.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 20, 2015

    Hachana na ufayatu: Hii ni nguvu kazina pia wapiga Kura! Vizuri na kuona wanfanya kazi na kuinua Uchumi wa Sumbawanga na Kigoma!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...