MWL. ERNEST MWAMKAI KIONDO
Mpendwa Baba, tarehe 22 May 2015 umetimiza mwaka mmoja tangu ututoke hapa duniani kwa mapenzi yake Mwenyezi Mungu.
Mpendwa Baba, tarehe 22 May 2015 umetimiza mwaka mmoja tangu ututoke hapa duniani kwa mapenzi yake Mwenyezi Mungu.
Tunakukumbuka sana kwa malezi, upendo na ushauri wako ambao daima ndio dira yetu na kumbukumbu yetu.
Unakumbukwa sana na Wazazi wenza Mama Anna na Mama Agatha, Dada zako na sisi wanao, wakwe zako, wajukuu wote pamoja na ukoo wote wa Kiondo, Bendera, Mbaruku, Msangazi, Bila, Mjata na Nyangasa.
Japo haupo tena pamoja nasi kimwili, lakini kiroho tuko pamoja nawe kila siku.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu aendelee kukuhifadhi mahali pema peponi.
AMEN.
Kutakuwa na misa ya kumuombea Marehemu Mzee wetu Jumamosi tarehe 6/6/2015 katika Kanisa la Mtakatifu Yohana Krisostomo, Majani Mapana, Tanga.
Misa inategemewa kuanza saa 3 asubuhi na kabla ya hapo, Ijumaa tarehe 5/6/2015 kutakuwa na mkesha nyumbani kwa Marehemu Kwaminchi Tanga, karibu na Uwanja wa saba saba.
Karibuni sana.
MPENDWA BABA TUTAKUKUMBUKA DAIMA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...