Mwenyekiti wa chama cha Tnzania Labour Part (TLP) Agustino Mrema akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo) katika mkutano uiliofanyika kwenye ukumbi wa Idara ya Habari MELEZO kuhusu kukanusha kuwa yeye amefukuzwa TLP,Kushoto Mkurugenzi wa Msaidizi wa Idara ya Habari Maelezo,Kulia ni Katibu Mkuu wa TLP,Nancy Mrikariya.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
MWENYEKITI wa Chama cha Tnzania Labour Party (TLP) Agustino Mrema,amesema hajafukuzwa unachama katika chama hicho.
Mrema aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana kuwa yeye ni mwenyekiti wa Chama hicho na hakuna mtu wa kumtoa kutokana na kuendesha chama hicho kwa kufuata katiba.
Amesema kikundi kinachofanya hivyo na kusambaza taarifa kuwa kimemtoa kutokana na kufanya vikao hakitambui na kuwataka wanachama kuwabeza watu hao.
Mrema amesema yeye akiwa Mwenyekiti ataendelea kutetea jimbo lake la Vunjo,hivyo watu wanaosema amefukuzwa katika chama wapuuzwe.
Aidha amesema biashara ya Urais ameachana nayo ,sasa kazi yake ni Ubunge kupitia jimbo la Vunjo na ameweza kuleta maendeleo ya wananachi katika jimbo hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...