KAMPUNI za burudani nchini, Linda Media Solution (Limso), na The African Stars Entertainment (Aset), zimeunganisha nguvu katika kuandaa shindano la kumsaka Kimwana wa Twanga Pepeta 2015.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Aset, Asha Baraka, alisema kampuni hizo zitashirikiana kuandaa shindano hilo ambako hivi sasa wameanza kusaka washiriki na habari zaidi zitatolewa hivi karibuni.
“Shindano hili ambalo tumepanga lifanyike baadaye mwaka huu jijini Dar es Salaam, tutatoa taarifa mahali ambapo warembo hao wataweza kuchukua fomu za kushiriki,” alisema.
Alifafanua kuwa katika shindano hilo kutakuwa na mizunguko mitatu na baadaye fainali, ambako zawadi nono itatolewa kwa mshindi.
Aidha, alitoa wito kwa wadhamini kutoa ushirikiano, kwani shindano hilo huwa lina mvuto wa aina yake na kushirikisha kina dada warembo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...