Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Maalim Seif Sharif Hamad amewataka Wazinzibari kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura linalotarajiwa kuanza Mei 16 mwaka huu, ili waweze kutumia haki zao kikatiba za kushiriki uchaguzi mkuu kwa kupiga kura.
Maalim Seif Sharif Hamad ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF),amesema kuwa uchaguzi mkuu uliopita ulikuwa wa uhuru na wa amani lakini ulikuwa na kasoro katika daftari la wapiga kura, kwamba wapiga kura walikuwa na kadi mbili hali ambayo kwa sasa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) inapaswa kuliangalia jambo hilo kwa umakini.
Amesema kuwa katika kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) ipitie upya wapiga kura kwa kutumia mfumo wa kieletroniki kuhakiki makosa yaliyokuwa yakijitokeza kwa watu kujiandikisha mara mbili.
Maalim Seif amesema kuwa katika kasoro hizo ZEC iharakishe kutangaza majimbo ya uchaguzi kutokana na kazi hiyo ilishafanywa muda mrefu kupitia Wizara ya Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ.
Amesema katika kasoro zilizokuwemo kwenye daftari la wapiga kura ni pamoja watu waliofariki kuendelea kupiga kura kutokana na mfumo huo wa kutohakiki wapiga kura pamoja na watu wasio wakazi wa Zanzibar kupiga kura.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar,Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na Waandishi wa habari katika
Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo,juu ya harakati za kuelekea Uchaguzi
Mkuu Zanzibar, kulia ni Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano ya Umma, Salim
Biman na kushoto ni Naibu katibu Mkuu Zanzibar (CUF),Nassoro Ahmed Mazrui.

Mkurugenzi wa mambo ya Nje wa CUF Ismail Jussa, akijibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika leo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa kitengo cha Sera,Utafiti na Mafunzo, Hassan Jani Masoud akielezea juu ya utafiti walioufanya kupitia kitengo hicho cha CUF juu ya changamoto ya daftari la wapiga kura Zanzibar katika mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya waandishi habari wailiohudhuria katika mkutano na ulioitishwa na Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Maalim Seif Sharif Hamad
,(PICHA NA EMMANUEL MASSAKA,GLOBU YA JAMII).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...