Na Avila Kakingo,Globu
ya Jamii.
CHAMA cha Wanawake Wanasheria Tanzania (TAWLA)
wamefanya maadhimisho ya miaka 25 ya
kujenga uwezo na kufanya uchechemuzi juu ya haki za wanawake, tangu kuanzishwa kwake mwaka 1990 hapa nchini.
Akizungumza katika uzinduzi wa Maadhimisho ya
Chama hicho yaliyofanyika katika ukumbi wa jengo la YWCA jijini Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake wanasheria
(TAWLA), Magreti Ringo amesema kuwa chama hicho kimefanikiwa kutoa msaada wa
kisheria kwa wanawake wasiopungua milioni tano kupitia vituo vilivyopo Dar es
Salaam,Tanga,Arusha na Dodoma.
Pia chama hicho kimefanikiwa kutoa mafunzo kwa
wasaidizi wa kisheria 402 ili kuhakikisha jamii inapata msaada wa kisheria na kuhamasisha
jamii, kujua masuala ya kisheria kupitia machapisho mbalimbali.
Ringo amesema kuwa chama chicho kinaratibu muungano wa jukwaa la jinsia la katiba, ambalo limefanya
kazi na kuchangia kuwepo kwa ibara nyeti zinazolinda haki za kijinsia kwenye
katiba inayopendekezwa.
Katika maadhimisho ya miaka 25 ya chama hicho kimehamasisha uandikaji wa wosia bila gharama
yeyote.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...