Na Bashir Yakub.
Makampuni ya simu kama Vodacon, Airtel, Tigo, Zantel, Sasatel, na mengineyo yamekuwa yakitenda makosa mbalimbali kwa wateja wao. Mara kwa mara wateja wa simu wamekuwa wakilalamikia matendo ya makampuni haya lakini wengi wao wamekuwa hawachukui hatua zaidi ya kulalamika. Ni watu wachache mno ambao wamekwishachukua hatua za kisheria dhidi ya makampuni haya licha ya uonevu mkubwa wa kihuduma wanaousababisha. Ukiangalia kwa haraka utaona kuwa walio wengi hushindwa kuchukua hatua kwanza kwa kutojua kama kuna uwezekano wa kuchukua hatua , pili kutokujua kama kilichotendeka ni kosa na kinahitaji adhabu au wakati mwingine kwa kuamua kuacha tu.
1.MNIGERIA ALIPWA USD 90,000 KWA KOSA LA KAMPUNI YA SIMU.
Nchi kama marekani, uingereza na karibia nchi nyingine za ulaya zote, na Afrika zaidi Nigeria na Afrika kusini makampuni ya simu yamekuwa yakilazimika kulipa fidia nyingi mara kwa mara kwa wateja wao kutokana na makosa mbalimbali ambayo makampuni yamesababisha kwa wateja. Hivi karibuni nchini Nigeria kampuni moja ya simu imelazimika kumlipa fidia ya USD 90,000 mtu mmoja ajulikanaye kwa jina la Edo Emeka baada kuishtaki kampuni hiyo kwa kumfungia kadi/namba(line) yake pasi na sababu za msingi.
Katika kesi hiyo mlalamikaji Emeka aliieleza mahakama kuu mjini Lagos usumbufu alioupata kwa kitendo hicho cha kufungiwa namba yake kitendo kilichopelekea mahakama iamuru alipwe tuzo(decree) hiyo. Aidha zipo kesi nyingi katika nchi mbalimbali ambapo watu wamelipwa mamilioni ya pesa kutokana na makosa yanayosababishwa na makampuni haya. Hapa kwetu makampuni haya hutengeneza faida tu na sisi hatuyawajibishi kwa namna yoyote kwa makosa na usumbufu tunayosababishiwa kila siku.
2. KWA MAKOSA HAYA WAWEZA KUISHTAKI KAMPUNI YA SIMU.
Hapa kwetu sawa na nchi nyingine duniani makosa ya makampuni ya simu kwa wateja wao hufanana. Kuna kufunga namba ya mtu bila sababu za msingi, kukata salio la mtu bila sababu za msingi, kumwekea mtu mwito wa simu ambao yeye mwenyewe hajachagua , kutumia mziki wa msanii katika program yoyote bila ridhaa yake , kutokuwa hewani au kukata mawasiliano bila taarifa kwa wateja, majenereta ya minara kusabababisha usumbufu na kelele kwenye makazi ya watu, kwa kutaja ni machache.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...