Mbunge wa Mvomero na Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla ameendelea kuchangiwa fedha za kuchukua fomu ya kuwania Ubunge wa Jimbo hilo pamoja na kufanya kampeni na makundi mbalimbali wilaya ya Mvomero, na safari hii ni umoja wa wanawake wa CCM (UWT) tawi la madizini na kushirikisha matawi kumi kata ya Mtibwa na kata ya Diongoya.

Katika mkutano mkubwa wa kihistoria wanawake wa matawi walimtaka mbunge huyo wakati ukifika achukue fomu na wao wanamuahidi ushindi ndani ya chama na nje ya chama.

Akisoma risala kwa niaba ya akina mama hao katibu wa tawi jumuiya ya wanawake Tawi la madizini  Bi. Mariam Mdabwa alieleza kuwa Mbunge wao amekuwa mstari wa mbele kusaidia akinamama wajasiriamali, Vijana na kuboresha huduma za Afya, elimu, umeme na maji katika jimbo la Mvomero hivyo umoja wa wanawake unamuomba uchukue fomu na walikabidhi Fedha sh 150,000 za kuchukulia fomu.

Akijibu risala hiyo mbunge wa Mvomero na Naibu Waziri wa Maji aliwashukuru na kuwaahidi muda ukifika atachukua fomu na pia aliwashukuru kwa mchango wa Fedha na kueleza awali alichangiwa fedha sh 2,309,000 na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha manyinga
 Mbunge wa Mvomero na Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akilakiwa na wananchi wa Jimbo lake la Mvomero wakati alipofika kuzungumza nao.
 Mbunge wa Mvomero na Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akitoa hotuba yake.
Mbunge wa Mvomero na Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akionyesha fedha alizochangiwa na Umoja wa Wanawake wa CCM tawi la madizini kwa ajili ya fomu ya ubunge.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 04, 2015

    Hivi huku kuchangiwa fedha kwa wagombea kuchukua fomu ambako tumekuwa tunakusikia sio kwa huyu mgombea peke yake, je mtu akichangiwa zaidi ya shilingi elfu hamsini si ukiukwaji wa sheria ya maadili kweli? Mwanasheria wa Blog atuelimishe hapa..

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 04, 2015

    Huu usanii wa kuchangiwa fedha umeanza anzaje?

    Maana sasa kila kitu mchango: elimu, harusi, msiba, graduation, ubunge utarajiwa, he huo mshahara utabaki vipi kwa matumizi ya nyumbani?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...