Na Anna Nkinda – Lindi

Vijana mkoani Lindi wametakiwa kuwa wazalendo na kutobaguana bali wasambaze upendo na kujiona wote ni sawa kwa kufanya hivyo wataondoa chuki na kudumisha amani, mshikamano na umoja katika jamii inayowazunguka.

Mwito huo umetolewa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akifungua klabu zalendo zilizopo katika  Manispaa ya Lindi.

Mama Kikwete ambaye ni Mke wa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alisema kama jamii itajenga tabia ya ubaguzi italeta chuki na upendo utatoweka na hivyo kusababisha vurugu zitakazopoteza  amani iliyopo.

Alisema uzalendo ni kiini cha maendeleo hivyo huwezi kuwa mzalendo kama hupingi rushwa na matumizi ya madawa ya kulevya, hutunzi mazingira, hushiriki kuchangia utoaji wa damu salama na kutokuchangamkia fursa mbalimbali za maendeleo zilizopo katika jamii yako.

Mama Kikwete alisema, “Leo hii nimezindua klabu zalendo, Mzalendo ni mtu mwenye huruma na mtu anayeona thamani ya kitu alichonacho tunzeni vitu mlivyonavyo ikiwemo Amani ya nchi yetu na mjitoe kufanya kazi kwa bidii ili muweze kupata maendeleo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...