Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
Kampuni ya
Majisafi na Majitaka Dar es Salaam(Dawasco)imeanza
rasmi operesheni kuwakamata watu waliojiunganishia
maji kwa njia haramu.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco,Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema operesheni hiyo itafanyika kanda zote za jiji la Dar es
Salaam ikiwa ni kutaka jamii kuacha tabia hiyo.
Amesema kuwa
wizi wa maji unafanya watu ambao ndio wateja wa Dawasco kukosa maji na kupata
watu wasio wateja wakiwa wameunganisha maji kwa kiwango kikubwa.
“Hatuwezi
kuacha maji yawe yanaibiwa huku wateja wetu wanaolipia ankara zao wakikosa, ni
lazima hatua zichukuliwe kwa wale wote watakaobainika na wizi wa maji yetu”amesema Luhemeja.
Luhemeja
amesema kwa wale watakaotoa taarifa za mtu anayeibia Dawasco atapewa Sh.500,000 ambapo kufanya hivyo watamlinda
dhidi ya huyo mwizi wa maji.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco,Mhandisi,Cyprian Luhemeja akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani kuhusiana na operesheni ya wizi wa maji jijini Dar es Salaam.
Mheshimiwa Cyprian Luhemeja umekuja na mpango mzuri.
ReplyDeleteTunaomba pia ututazame wenye shida nyingine ya maji.
Wakazi wa Tabata eneo la ubayaubaya kwa Jijo, tuliunganishiwa mambomba ya wachina mwaka 2008, tangu wakati huo hadi leo maji hayajawahi kutoka hata siku moja.
Tumewahi kufuatilia katika ofisi za Tabata mara nyingi sana wametueleza wanafahamu tatizo hilo litashughulikiwa sasa huu mwaka wa saba jamani wameshindwa kutusaidia? Tulianza kuomba mmoja mmoja hadi kwa vikundi bila mafanikio.
Kuna baadhi yetu tuliomba kuunganishiwa maji na tukalipa malipo yote, mimi binafsi nililipa shilingi laki sita mwaka 2008 mwanzoni baadaye wakasema hawawezi kuniunganishia maji kwa sababu yatakuja ya mradi wa wachina na kweli walikuja wakatufungia wengi tu. Nilipofuatilia zaidi zile shilingi laki sita zinaingizwa kwenye bili wakanieleza nitakatwa mpaka zitakapokwisha. Sasa sijui nitakatwa lini maana hayo mambomba ya wachina hayajawahi kutoa maji hata yalipofungwa siku ya kwanza hayakudondosha hata tone moja la maji hadi leo.
Wote tuliounganishwa tumekuwa tukinunua maji kabla ya mwaka 2008 hadi leo.
Kwa heshima na taadhima mheshimiwa tusaidie kuangalia hili kwa kushirikiana na ofisi ya tabata wanayodai wanalifahamu tatizo. Jamani mtu akifahamu tatizo si anatakiwa kutafuta suluhisho?
Asante
Nawasilisha