Mke wa Rais
Mama Salma Kikwete akiteta jambo na Mama Maria Nyerere mara baada ya shughuli
ya kuaga mwili wa Marehemu John Nyerere huko Msasani jijini Dar es Salaam, Marehemu John anatarajiwa
kuzikwa Aprili 13, katika kijiji cha Butiama,Mkoani Mara.
Mke wa Rais
Mama Salma Kikwete akiwa pamoja na Mama Maria Nyerere na Mama Fatma Karume (wa
nne kutoka kushoto) pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro
wamesimama mbele ya jeneza wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa Marehemu John
Nyerere iliyofanyika Msasani jijini Dar es Salaam,Mwili wa Marehemu John
unatarajiwa kusafirishwa kesho kwenda Butiama mkoani Mara kwa mazishi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...