Na Chalila Kibuda,
Globu ya Jamii 

MARAIS wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wamelaani kitendo cha baadhi ya askari kufanya jaribio la kutaka kuipindua serikali ya Burundi.
Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam leo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe amesema  kuwa hali ya Burundi ni tete na kwamba japo linaonekana ni jambo dogo lakini linaweza kugharimu maisha ya watu. 
"Hivyo tunatakiwa tuvute subira...Tusubiri na sio kulitangaza suala hilo kiushabiki wakati wenzetu wana tatizo. Afrika haitaki tena mtu yeyote kwa sababu yeyote kuhalalisha kuchukua nchi kwa mtutu”, amesema Membe.

Amesema Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambalo lilikuwa na mkutano juzi na jana, litakaa tena wiki ijayo kujadili  ajili ya hali ya Burundi.

Membe amesema, Wakuu hao wataketi tena Jumatatu baada ya kupata tathimini na  watatoa taarifa ya kinachoendelea nchini Burundi, hivyo kwa sasa hawatazungumzia lolote.

Membe amesema kuwa hajui aliko Rais Pierre Nkurunzinza ambaye anadaiwa aliondoka nchini jana kurudi Burundi huku kukiwa na taarifa za kutokwepo kwa Rais huyo  katika nchi yake kufuatia jaribio la kupinduliwa na baadhi wa askari wa nchi hiyo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akizungumza na waandishi wa habari mapema leo asubuhi kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu J.K. Nyerere, jijini Dar es salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...