Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Bw. Nachoa Zacharia kulia akiongea na
ujumbe kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakati wa Maafisa hao walipokuwa
katika ziara ya mafunzo stadi za maisha,ujasiriamali na elimu ya uongozi kwa vijana wa Mkoa wa
Ruvuma, kushoto kwake ni Mkuu wa Chuo cha Vijana cha Sasanda kilichopo mkoani Mbeya Bw. Laurian
Masele.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Mh. Charles Mhagama akisisitiza jambo
kwa maafisa kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakati wa ziara ya mafunzo ya
stadi za maisha,ujasiriamali, mfuko wa Vijana na elimu ya uongozi kwa vijana wa Mkoa wa Ruvum, kulia
Afisa Vijana kutoka Wizarani Bi. Amina Sanga na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria Bi.
Ester Riwa.
Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, na Michezo Bi. Amina Sanga akitoa mada ya jinsi ya
Vikundi vya vijana wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea vilivyokidhi vigezo vinavyoweza kunufaika na
mfuko huo,mafunzo hayo yamefanyika mkoani Ruvuma.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria Bi. Ester Riwa akitoa mada juu ya Sera ya Maendeleo ya
Vijana ya Mwaka 2007, Stadi za Maisha na ujasiriamali kwa Vijana wa Halmashauri ya Manispaa ya
Songea Mkoani Ruvuma.(Picha na Benjamin Sawe).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...