Mashimozz katika barabara hii ya Migombani, inayotokea DriveIn (makao makuu ya Zantel) kuelekea Victoria (Kairuki Hospitali) mpaka Makumbusho jijini Dar es salaam, yamekuwa ni kero kwa watumiaji wa njia hiyo, hasa kutokana na ukubwa wa mashimozz yaliyopo kwenye barabara hiyo. huo mpishano wa vyombo vya usafiri hapo pichani, si kwamba unatokana na mbwembwe za madereva, la hasha ni kutokana na namna ya kuyakwepa mashimozz hayo yaliyosheheni katika barabara hiyo.
 Hivi ndivyo hali ilivyo katika barabara hiyo hizi sasa, na hii ni kutokana na mvua zilizonyesha hivi karibuni. maana kabla ya hapo mambo yalikuwa mswano kabisa.
 Hapa ni mwendo wa staili ya kinyonga, maana wenye kwenda mbio huku hakuwafai kabisa.
 Hii gari imekwama baada ya kunasa kwenye shimo la Chemba iliyofumuka kutokana na kuzidiwa na maji, hivyo hapo kuna shimo kubwa sana ambalo liko wazi.hivyo watumiaji wa njia hii kuweni makini sana na hapo maana haijulikani ni lini mkandarasi atapita na kuja kufanya mambo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...