Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO Assah Mwambene akizungumza na waandishi wa habari (hawapo) ndani ya ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Msahuri,kumbukumbu za ukombozi wa Barani  Afrika,Daniel Ndagala, Mshauri na mtafiti UNESCO Phelippe Roisse na  wa mwisho ni Dinah Mumbaga Mtafiti na mshauri wa UNESCO.(Picha na Avila Kakingo).

Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

WAZIRI wa Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Mh.Bernard Membe anatarajiwa kuwa mgeni rasmi  katika uzinduzi wa maadhimisho ya   wiki ya Ukombozi Barani Afrika, maadhimisho hayo yatazinduliwa katika ukumbi wa  mikutano wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam Mei 25 mwaka huu.

 Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO Assah Mwambene wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na maadhimisho hayo ya  wiki ya  Ukombozi Barani Afrika.

Mwambene amesema kuwa  Serikali ikishirikiana na  shirika la  Umoja wa mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), watazindua Mradi wa Nyaraka za Urithi wa Tanzania(TAHAP), ambao ukikamilika utakuwa unaweka na kutunza kumbukumbu za nyaraka  mbalimbali zinazohusu Ukombozi Barani Afrika.

Amesema kuwa miongoni mwa matukio muhimu katika maadhimisho hayo ni pamoja na mdahalo unahohusu mchango wa vyama vya siasa katika harakati za  ukombozi utakaoongozwa na Dk. Salim Ahmed Salim, Profesa  Issa Shivji pamoja na Mh.Ibrahim Kaduma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...