Meneja Uendeshaji wa MultiChoice Tanzania, Ronald Baraka Shelukindo akizungumza machache wakati wa uzinduzi wa huduma ya kukodisha filamu iitwayo Box Office iliopo kwenye Dekoda ya Explora PVR, uliofanyika leo kwenye hoteli ya New Afrika, jijini Dar es salaam.
MultiChoice inapenda kuwatangazia wateja wa DStv kwamba, imezindua rasmi huduma ya kukodisha filamu ya Box Office leo tarehe 20 Mei 2015.
• Box Office ni huduma inayokuwezesha kukodisha na kuangalia filamu mpya ( Hazionyeshwi kwenye DStv kwa wakati huo) Utafarijika nyumbani kwako mbele ya Explora dekoda yako. Huduma hii inapatikana kwa wateja wenye Explora PVR waliolipia kifurushi Premium, Compact Plus au Compact .
• Box Office unaweza kukodisha Filamu kwa masaa 48, kwa kiasi kidogo cha malipo kwa kila filamu, Tunakuhakikishia kupata chaguo lako sababu kuna aina nyingi tofauti za Filamu.
• Unaweza kujiunga sasa na Box Office na kufurahia movie za Kimarekani, muda wowote utakapohitaji.
• Mteja atajiunga kwa tumia namba za kadi ya dekoda na kutuma kwenda namba 15111, Namba za kadi zitaonekana kwenye runinga yako wakati wa kujiunga.
• Kwenye Box Office, utapata zaidi ya Filamu 20 za kukodisha ,ni sababu jingine ya kukufanya ujiunge na Explora dekoda.
Njia za Malipo ya Box Office.
Mteja anaweza kuingiza malipo ya awali kwenye akaunti ya Box Office kupitia njia zilezile anazotumia kulipia akaunti ya malipo ya mwezi ya DStv. Malipo hayo yatatumika kila mara pale mteja atakapokodisha Filamu kwenye Box Office. Gharama ya kukodisha Filamu ni Tsh.4,400 tu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...