Na Ismail Ngayonga
MFUKO wa wakfu wa kuendelezazao la Korosho nchini umetenga kiasi cha Tsh. Bilioni 6 kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vitatu vya kubangulia korosho vitakavyojengwa katika Wilaya za Mtwara, Tunduru na Mkuranga.
Taasisi zitakazojenga viwanda hivyo ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kupitia Kitivo cha Biashara na Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU).
Akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa mikataba baina ya mfuko huo na wataalamu washauri jana (Jumatano Mei 6, 2015), Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfukohuo, Athuman Nkinde katika bajet iiliyopo kiwanda kimetengewa kiasi cha Tsh Bilioni 2 na pia fedha hizo zinatarajia
kuongezeka kila mwaka kulingana na mahitaji yatakavyojitokeza.
Nkinde alisema ujenzi wa viwanda hivyo unatarajia kuanza katika kipindi cha miezi mitatu ijayo ambapo pindi vitakapomalika kila kiwanda kinataraji kuzalisha tani 10000 kwa mwaka, na kuongeza kuwa Ofisi yake ina imani kubwakuwa ujenzi wa viwanda hivyo utasaidia kuleta mageuzi makubwa ya zao la koroho nchini.
Aliongeza kuwa madhumuni ya kuanzisha viwanda hivyo ni kuliongezea thamani zao la korosho ili liweze kuchangia kikamilifu katika kukuza uchumi wananchi pamoja na wakulima wa zao hilo nchini.
Kwa mujibu wa Nkinde alisema taasisi zilizopewa kazi ya ujenzi wa viwanda hivyo havina budi kutambua thamani ya viwanda hivyo, kwani zipo taasisi nyingi zikiwemo za umma na zile za sekta binafsi zilizoomba zabuni kwa ajili ya ujenzi huo.
“Tumeingia katika historia mpya leo hii, dunia nzim itasikia taarifa hizi za ujenzi wa viwanda hivi, hivyo ni wajibu wenu kufanya kazi kwa kuzingatia uwezo wa kitaaluma mliokuwanao” alisemaNkinde.
“Tanzania imekuwa ikisafirisha nje ya nchi korosho ghafi, kwa kujenga viwanda hivi kutatusaidia kupunguza gharama hizo sambamba na kuongeza thamani ya zaohilo” alisema Nkinde
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Mfuko huo, Suleiman Lenga aliwataka wataalamu washauri hao kuzingatia viwango, ubora na muda katika kutekeleza ujenzi wa miradi hiyo kwani taasisi hizo zina uzoefu mkubwa katika kusimamia na kundeleza miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.
Alisema katika mikataba iliyosainiwa, Chuo cha Ardhi kitahusika zaidi katika kuandaa michoro, ramani na usanifu wa majengo wakati, Chuo cha Biashara kitahusika katika kuandaa andiko la mradi litakalohusiana na masuala mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa masoko.
Naye Mwadili wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika Kitivo cha Biashara, Dkt. Ulingeta Mbamba alisema taasisi itafanya kazi kwa weledi mkubwa ili kuhakikisha kuwa ujenzi huo utafikia katika ubora na viwango vilivyokusudiwa.
“Zao la korosho limekuwa kwa sasa limekuwa ni zao muhimu kwa uchumi wa Tanzania na wananchi kwa ujumla, hivyo tutahakikisha kuwa kupitia ujenzi huu zao hili linazidi kuongezewa thamani yake” alisema Dkt. Mbamba.
Aidha Makamu Mkuu wa Taaluma katika Chuo Kikuu cha Ardhi, Prof. Gabriel Kassenga alisema wa Chuo kitahakikisha kuwa viwanda hivyo vitaleta tija kwa kukuza uchumi wa Taifa na wakulima wa zao la koerosho nchini.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Nchini,Mundhir Mundhir
akizungumza na waandishi wa habari (hawapopichani) leo Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya utiaji saini wa mikataba ya ujenzi wa viwanda vitatu vya kubangulia korosho katika Wilaya za Mtwara, Tunduru na Mkuranga kati ya Mfukowa Wakfu wa kuendeleza Zao la Korosho Nchini na wataalamu washauri kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi cha Jijini Dar es Salaam na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Kitivo cha Biashara. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Mfuko huo Bw.SuleimanL enga.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa wakfu wa kuendeleza Zao la Korosho Nchini Bw. Athuman Nkinde akizungumza na waandishi wa habari (hawapopichani)Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya utiaji saini wa mikataba ya ujenzi wa viwanda vitatu vya korosho katika Wilaya za Mtwara, Tunduru na Mkuranga kati ya Mfuko huo na wataalamu washauri wa kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi cha Jijini Dar es Salaam na Shule ya Elimu ya Biashara katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Kitivo cha Biashara . Katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania, Bw. Mundhir Mundhir na Katibu Mtendaji wa mfuko huo Bw. Suleiman Lenga.
Mwadili wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kitivo cha Biashara, Dkt. Ulingeta Mbamba (kushoto) na Katibu Mtendaji wa Mfuko wa wakfu wa Kuendeleza zao la Korosho Nchini, Bw. Suleiman Lenga wakionyesha mkataba wa ujenzi wa viwanda vitatu vya korosho katika Wilaya za Mtwara, Tunduru na Mkuranga. Hafla hiyo ilifanyika leoJumatano (Mei 6, 2015) Jijini Dar es Salaam.
1 Makamu
Mkuu wa Chuo cha Ardhi cha Jijini Dar es Salaam, Prof. Gabriel Kassenga (kulia)
na Katibu Mtendaji wa Mfuko wakfu wa Kuendeleza zao la Korosho Nchini, Bw.
Suleiman Lenga wakionyesha mkataba wa ujenzi wa viwanda vitatu vya korosho katika
Wilaya za Mtwara, Tunduru na Mkuranga. Hafla hiyo ilifanyika leo Jumatano (Mei
6, 2015) Jijini Dar es Salaam. (PICHA NA ISMAIL NGAYONGA- MAELEZO)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...