Kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha maeneo mbali mbali hapa jijini Dar, imepekea baadhi ya njia kufungwa kutokana na wingi wa maji kwenye baadhi ya madaraja, hali iliyopelekea kuwepo kwa msongamano mkubwa la magari kama ionekanavyo pichani hapa katika Barabara ya Azikiwe, kutokea kwenye kipita shoto cha Askari.Picha zote na Othman Michuzi.
 Mjini leo hakuna kutoka, maana foleni ni kila kona.
 Azikiwe hiyo.

Mzee wa Feva kaamua kukaa kando, maana hakuna hata anaetaka kumsikiliza.
 Barabara ya Ohio street nako mambo ni kama hivi.
 Trafiki wa kujitolea akizizuia gari zisiingie katikati ya barabara kuhofea kuendeleza msongamano.
 Baadhi ya Madereva wa magari yaliopo kwenye msongamano wakimsikiliza mzee wa Feva juu ya hali ya barabara.
 Mtaa wa Chimala 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 07, 2015

    Dah poleni sana wa-tz kwa mateso mazito mnayoyapata ya kukaa kwenye mafoleni yasiyo na mwisho!.nasikia siku hizi ni kawaida sana kukaa kwenye foleni masaa hata manne!.ona mji hauna mpangilio nyaya za umeme zipo hovyo hovyo njiani, barabara very poor designed...hivi kuna ma-injinia huko?

    Ufisadi, wizi, ujangili, ubinafsi, uzembe,u-mimi,ulafi, etc umeifikisha nchi hali hiyo!.kwa hali hii hata wenye pesa hawa-enjoy huko bongo! ndo mana sisi huku mamtoni hatutaki kurudi as life is too short to suffer!.wazee wetu walisuffer kupata uhuru why na sisi tuendelee kupata mateso katika kuishi kwenye nchi huru!

    Ankal ndugu yangu nakukaribisha tena mamtoni upate raha angalau kwa miaka michache uliyobakiza kuishi maana life ya bongo imepunguza sana maisha yako!.ukiwa tayari nishtue ankal nitakutumia ticket na kuandaa sehemu ya kufikia kwa miezi sita ya mwanzo.

    mdau

    Washington DC

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 08, 2015

    Tnahitaji trams na underground miaka ya hivi karibuni vyuo vikuu vianze michoro kama haipo.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 08, 2015

    nauliza haya ndo maendeleo ya kila mtanzania kuwa na gari na bara bara za kupita hakuna msogamano wa magari kama haya.
    nauliza tena haya ndo maendeleo au ujinga tu.wenzenu wana kuwa na bara bara za juu kwa juu na kila sehemu huoni foleni kama hizi.vichwa maji tu what a shame?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...