RAis mstaafu wa awamu ya tatu Mhe. Benjamin Mkapa akifungua Mkutano wa mwaka wa Bodi ya Usajili wa Wakandarasi leo jijini Dar es salaam
  Baadhi ya Wahandisi waliohudhuria mkutano huo wakiapishwa leo jijini Dar es Salaam. 
  Washiriki wa mkutano huo wakifuatilia masuala mbalimbali. Picha/Aron Msigwa -MAELEZO. 

Na Aron Msigwa, 
MAELEZO .


Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mhe.Benjamin Mkapa amewataka Wakandarasi kote nchini kufanya kazi zao kwa weledi na kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia Sekta ujenzi ili miradi wanayoisimamia na kuitekeleza iweze kuwa na manufaa kwa taifa.

Mhe.Mkapa ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa Bodi ya Usajili wa Wakandarasi (CRB) uliowawajumuisha pia wadau wa sekta ya Ujenzi kutoka nchini Malawi na Kenya.

Amesema umakini katika usimamizi wa kazi za wakandarasi na uwepo wa wataalam waliobobea katika sekta ya ujenzi umechangia kwa kiasi kikubwa kasi maendeleo inayotokea sasa nchini Tanzania.
Ameeleza kuwa sekta ya ujenzi ndiyo iliyolifikisha taifa hapa kutokana na mchango wake katika Pato la Taifa unaofikia asilimia 14.1 ikifuatiwa na sekta nyingine na kuongeza kuwa ili nchi iweze kuendelea lazima wakandarasi wazalendo wajengewe uwezo ili kuhakikisha kuwa fedha zinazotolewa katika sekta ya ujenzi zinabakia Tanzania na kuwanufaisha wazawa badala ya wageni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...