Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) tarehe 25 Mei, 2015 kuhusu Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unaotarajiwa kufanyika Jijini Dar es Salaam tarehe 31 Mei, 2015 kuhusu masuala ya amani na usalama nchini Burundi. Mkutano huo ambao umeitishwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya EAC, Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete utatanguliwa na Mkutano wa Baraza la Mawaziri.
Mhe. Membe akiendelea na mkutano wake na Waandishi wa Habari.Picha na Reginald Philip

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 26, 2015

    Kikwete Mwambie Nkurunzinza kuwa sasa basi! Aondoke. Watu wamechoka kupokea wakimbizi bila ya kuwa na sababu ya maana! Nkurunzinza ndio tatizo!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...