
Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Mh. Fadhil Nkurlu
(kushoto) akimhoji dereva wa lori aliyejitambulisha kwa jina la Bw. Kabyemela
(mwenye tisheti jekundu) baada ya kuwekewa mtego na kukamatwa na shehena ya ngozi
ya magendo iliyokuwa ikisafirishwa kuelekea nchi jirani. Shehena hiyo
ilikamatwa katika kizuizi cha Kyaka.
Baadhi ya ngozi ya magendo iliyokamatwa baada ya Mkuu huyo wa
Wilaya kuweka mtego kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama. Shehena
hiyo ya ngozi ya magendo inakisiwa kufika uzito wa takribani tani 10.
Missenyi. 8 Mei, 2015 - Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Mh. Fadhil
Nkurlu amekamata shehena kubwa ya ngozi ya magendo yenye uzito unaokisiwa tani
10 ikisafirishwa kwenda nje ya nchi bila kibali wala nyaraka zozote za
serikali.
Kwa mujibu wa taarifa za ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Missenyi ngozi
hiyo ilitokea Kahama ikiwa inaelekea nchini Uganda na ilikamatwa katika kizuizi
cha Kyaka, wilayani Missenyi.
"Tulipata taarifa kutoka kwa raia wazalendo tangu jana yake
kwamba kuna bidhaa za magendo ambayo huwa yanapita usiku, ndipo nikawapanga
vijana kutoka vikosi vyote vya ulinzi na usalama kuweka mtego huu,"
alisema DC Nkurlu.
"Hiki ni kipindi ambacho magendo ya kahawa husafirishwa kwa
wingi kwenda nje ya nchi na hivyo hukosesha serikali mapato yake stahiki.
Lakini tumejipanga ipasavyo na tutahakikisha tunakamata kila aina ya magendo.
Hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayejihusisha katika
biashara hii," alisisitiza.
"Napenda kutoa rai kwa wananchi wote wa Missenyi kuendelea
kutoa ushirikiano wao kwa serikali ili kuweza kukamata bidhaa hizi za magendo
na kudhibiti mtandao huu haramu," alisema Mh. Nkurlu.
Hii ni mara ya pili ndani ya wiki hii magendo yanakamatwa ambapo
Jumatatu shehena kubwa ya mbao zilikuwa zikisafirishwa kinyemela zilikamatwa na
bado zinashikiliwa katika kituo cha polisi cha Kyaka.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...