Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
WAZIRI wa Fedha na Uchumi, Saada Salum Mkuya anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 10 ya Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) yatakayofanyika Mei, 19 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi ya PPRA, Balozi Dk. Matern Lumbanga, amesema lengo la maadhimisho ni kukutanisha wadau wa manunuzi ya umma nchini kujadili mafanikio katika udhibiti wa manunuzi ya umma na changamoto wanazokabiliana nazo katika sekta hiyo.
Lumbanga amesema katika maadhimisho hayo kutafanyika warsha maalum ya wadau wa habari ambao ni waandishi ,wahariri wawakilishi wa kutoka Baraza la Habari Tanzania (MCT) pamoja na Umoja wa Klabu za waandishi wa habari Tanzania (UTPC) itakayofanyika Mei 18 ukumbi wa Diamond Jubilee.
Amewataja wahusika katika uzinduzi wa maadhimisho hayo kuwa ni Wakandarasi,Wataalam wa Ushauri,Watoa Huduma katika sekta hiyo,Wagavi na Taasisi Nunuzi ,wanasiasa asasi za kiraia wanataaluma, wanafunzi wanaosomea taaluma ya manunuzi pamoja na wananchi kwa ujumla.
Lumbanga amesema katika maadhimisho hayo Mei 20 itakuwa ni maalumu kwa wadau wa manunuzi kutoka Halmashauri zilizoko katika Mikoa ya Dodoma,Pwani,Tanga,pamoja na Kigoma ikiwa ni mpango wa kuzijengea uwezo wa manunuzi chini ya miradi inayofadhiliwa na serikali ya Ubelgiji.
Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni Miaka 10 ya PPRA,Tumethubutu ,Tumeweza ,Tushirikiane kuboresha zaidi manunuzi ya Umma, hivyo wadau wote wa manunuzi ya umma kutoa ushirikiano chanya katika kuzuia upotevu wa fedha za umma kwenye manunuzi yasiyo na tija.
Mwenyekiti wa Bodi ya PPRA, Balozi Dk. Matern Lumbanga akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maandimisho ya miaka 10 ya PPRA katika ukumbi wa mikutano wa Mamlaka hiyo leo jijini Dar es Salaam leo, kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, Laurent Shirima.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria katika mkutano na Mwenyekiti wa Bodi ya PPRA leo jijini Dar es salaam. Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...