Na Maryam Kidiko-MaelezoZanzibar
Mwanaharakati wa
Masuala ya Wanawake wa Jimbo la Mwana kwerekwe Bi Rihi Haji Ali amewataka Wanawake
wenzake kujitokeza kwa wingi kugombania
nafasi mbali mbali za Uongozi ili kuweza kutetea haki zao .
Hayo
ameyasema huko Mwanakwerekwe wakati akizungumza
na Waandishi wa habari katika suala zima la wanawake kuacha woga na kujitokeza
kwa wingi kugombania ili waweze kujisemea wenyewe na kupata haki zao za
kimsingi.
Hata hivyo
amesema wakati umefika kwa Wanawake kujisemea wenyewe na kuacha tabia ya
kusemewa matatizo yao jambo ambalo linarudisha nyuma na kuchelewa kupata haki
zao za msingi wanazokusudia.
Amesema kuwa
Wanawake watapojitokeza kwa wingi na kuwa na ushirikiano mkubwa wataweza
kutetea haki zao za msingi hasa katika suala zima la udhalilishaji unaojitokeza
hapa Nchini kwa wanawake hao.
Vile vile
amesema indapo watajitokeza Wanawake kugombani nafasi hizo watatoa ushirikiano
mkubwa wa kumpigia kura ili kuwapa hamasa wanaume na wao waweze kuwaunga mkono katika
kugombania nafasi hizo.
“Mwanamke
yoyote akijitokeza kugombania Uongozi tutatoa ushirikiano mkubwa na kuhakikisha
anapita katika ushindani huo”Amesema mwanaharakati huyo. Amefafanuwa kuwa
wanajitahidi kutoa Elimu sehemu mbali mbali na kuwaelimisha Wanawake jinsi ya
kugombea na kuacha imani potofu zinazosemwa Katika Jamii.
Hata hivyo
amesema wataunda Kamati Ndogo ndogo ili kuhakikisha kila Mwanamke aliyekuwa na
vigezo vya kugombania nafasi yoyote ya uongozi kuweza kupata nafasi hiyo.
Mwanaharakati
huyo ameishukuru Jumuiya ya Waandishi
wa habari Wanawake Tanzania (TAMWA)
pamoja na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Kwakuweza kuwatetea Wanawake na
kuhakikisha wanapata haki zao za msingi.
Sambamba na
hayo amevitaka Vyombo vinavyotoa Elimu
kuhusu masuala ya Wanawake na kuzidi kutoa Elimu kwa Wanawake na kuwataka Wanawake
kutoa mashirikiano pamoja na kupendana ili kutimiza lengo walilokusudia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...